Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 09:17

Hali ya tahadhari yatangazwa na waziri mkuu Haiti


Polisi wa Haiti wakitafuta ushahidi nje ya nyumba ya rais.(Picha na VALERIE BAERISWYL / AFP).
Polisi wa Haiti wakitafuta ushahidi nje ya nyumba ya rais.(Picha na VALERIE BAERISWYL / AFP).

Mitaa ya mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, ilikuwa mitupu Jumatano, kufuatia kuuawa kwa Rais Jovenel Moise

Mitaa ya mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, ilikuwa mitupu Jumatano, kufuatia kuuawa kwa Rais Jovenel Moise katika makazi yake binafsi mapema asubuhi. Biashara zilifungwa, watu wengi walibaki majumbani na magari ya polisi yenye silaha yalionekana kwenye barabara kuu. Askari wenye silaha walikuwa wakilinda katika maeneo muhimu ya mji mkuu.

Hali ya tahadhari imetangazwa na Waziri Mkuu wa mpito Claude Joseph, ambaye alisema ndiye mkuu wa nchi kwa sasa.

Maafisa wa Haiti wanasema watu wenye silaha nzito wakijifanya kama Maafisa wa kupambana na Dawa za kulevya wa Marekani ambao walizungumza Kihispania na Kiingereza walimpiga risasi na kumuua rais katika shambulio lililoratibiwa kwa hali ya juu. Mkewe, Martine Moise, alijeruhiwa vibaya na bado yuko katika hali mbaya lakini thabiti kwenye hospitali ya Miami.

Mkuu wa Jeshi la Polisi la kitaifa Léon Charles aliwaambia waandishi wa habari jana jioni kuwa mamluki wanaoshukiwa kutekeleza mauaji ya Moise waliuawa katika majibizano ya risasi na polisi, na washukiwa wengine wawili walikamatwa.

Charles alisema maafisa watatu wa polisi walioshikiliwa mateka na washukiwa wauaji waliachiliwa huru. Hakutoa habari yoyote juu ya operesheni hiyo.

XS
SM
MD
LG