Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 09:18

Rais wa Haiti Jovenel Moise ameuawa na watu wasiojulikana


Rais wa Haiti, Jovenel Moise
Rais wa Haiti, Jovenel Moise

Katika taarifa, Joseph alisema kundi la watu wasiojulikana  walihusika na mauaji hayo, ambayo aliyaita kitendo cha kuchukiza, kisicho cha kibinadamu na kishenzi

Rais wa Haiti, Jovenel Moise ameuawa kwa kupigwa risasi, katika shambulizi lililotokea kwenye makazi yake binafsi, waziri mkuu wa mpito, Claude Joseph alisema Jumatano.

Katika taarifa, Joseph alisema kundi la watu wasiojulikana walihusika na mauaji hayo, ambayo aliyaita kitendo cha kuchukiza, kisicho cha kibinadamu na kishenzi.

Alisema pia mke wa Moise, Martine alijeruhiwa na kupelekwa hospitali kwa matibabu. Haiti imekuwa ikishuhudia udhaifu wa kisiasa na mgawanyiko pamoja na ongezeko la ghasia za magenge.

XS
SM
MD
LG