Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:50

Waziri mkuu wa Haiti kujiuzulu


Kaimu waziri mkuu wa Haiti Claude Joseph
Kaimu waziri mkuu wa Haiti Claude Joseph

Afisa mmoja wa serikali ya Haiti amesema Jumatatu kwamba waziri mkuu wa muda, Claude Joseph ambaye amekuwa akiendesha taifa tangu kuuwawa kwa rais Jovenel Moise atajiuzulu ili kutoa nafasi kwa mtu aliyekuwa ameidhimishwa na na kiongozi huyo kabla ya kifo chake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, serikali mpya itaanza kufanya kazi Jumanne, bila ya kuwa na rais wakati ikitarajiwa kuitisha uchaguzi haraka iwezekanavyo.

Kabla ya kuuwawa kwake hapo Julai 7 wakati akiwa kwake nyumbani kwenye mji mkuu wa Port au Prince, Moise alikuwa ameidhinisha Ariel Henry kuchukua nafasi ya Joseph kama waziri mkuu.

Serikali ya Marekani imesifu hatua hiyo ikisema kuwa inaridhika kuona viongozi wa kisiasa pamoja na wale wa kiraiya wakishirikiana ili kuunda serikali itakayohakikisha udhabiti wa taifa.

Sasa hivi Haiti haina bunge la kutegemewa wala mfumo wa kupokezana madaraka, suala ambalo limezua uhasama wa kisiasa na kiusalama nchini humo kwa muda sasa.

Inakisiwa kuwa mauwaji ya Moise aliyekuwa na umri wa miaka 53 yalikiwa ya kisiasa. Ripoti zimeongeza kusema kuwa kwa sasa Haiti itabaki bila rais hadi pale uchaguzi utakapofanyika.

XS
SM
MD
LG