Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:33

Haiti : Polisi yamkamata mshukiwa anayehusishwa na kundi lililomuua Rais


Mkuu wa idara ya Polisi ya Kitaifa Leon Charles.
Mkuu wa idara ya Polisi ya Kitaifa Leon Charles.

Polisi nchini Haiti wamemkamata mtu ambaye anashukiwa kuwa kiongozi wa kundi lililomuua Rais Jovenel Moise, wiki iliyopita.

Mamlaka zinamshutumu Christian Emmanuel Sanon kwa kuajiri mamluki kwa nia ya kumwondoa Rais Moise madarakani na kupanga njama za kuchukua nafasi ya rais huyo.

Mkuu wa idara ya Polisi ya Kitaifa, Leon Charles, aliuambia mkutano na waandishi wa habari kwamba Sanon, mwenye umri wa miaka 63, alisafiri kwenda Haiti kwa ndege binafsi mapema mwezi Juni akifuatana na walinda usalama walioajiriwa na akinuia kuchukua nafasi ya rais.

Charles ameeleza kuwa : "(Christian Emmanuel Sanon) aliwasili Haiti kwa ndege binafsi kutimiza malengo ya kisiasa, kulingana na habari tuliyonayo. Kulingana na uchunguzi, aliwasiliana na kampuni ya huduma za usalama, kuwaajiri majambazi. Alifika Haiti mwanzoni mwa Juni, akifuatana na baadhi yao ambao hapo awali walipaswa kuhakikisha usalama wake. "

Polisi wanasema kile ambacho zamani kilikuwa dhamira ya kumlinda Sanon, baadaye kilibadilika na kuwa kutaka kuchukua nafasi ya rais.

Kufuatia mauaji hayo nyumbani kwa Moise Jumatano iliyopita, polisi waliwakamata raia kadhaa wa Colombia, na Wamarekani wawili wa asili ya Haiti, ambao, mamlaka zilisema ni wa kitengo cha makomando, wenye silaha nzito, na waliopewa mafunzo.

Kulingana na Jarida la Miami, washukiwa hao kutoka Colombia, walisema dhamira yao ilikuwa kumkamata Moise na wala siyo kumuua.

Polisi baadaye walithibitisha Sanon alikuwa amempa mmoja wa washukiwa hao, hati ya kukamatwa kwa rais.

Mauaji hayo yameitumbukiza Haiti, inayokumbwa na umasikini mkubwa, katika machafuko.

Serikali imetoa wito wa kulomba msaada kutoka jumuiya ya kimataifa.

Jana Jumapili, Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilisema wataalam kutoka FBI na Idara ya Usalama wa Ndani watasafiri kwenda nchini kusaidia uchunguzi.

XS
SM
MD
LG