Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:10

Marekani yajitayarisha kupokea wakimbizi wa Afghanistan


Baadhi ya wakimbizi wa Afghanistan muda mfupi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dulles jimboni Virginia
Baadhi ya wakimbizi wa Afghanistan muda mfupi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dulles jimboni Virginia

Utawala wa rais wa Marekani Joe Biden Jumatano umeanza kuwajulisha magavana wa majimbo pamoja na waratibu wa wakimbizi  kote nchini  kuhusu idadi ya wakimbizi wanaotarajiwa kwa kila jimbo miongoni mwa karibu 37,000 kutoka Afghanistan. 

Jimbo la California linatarajiwa kupokea zaidi ya wakimbizi 5,200 kulingana na takwimu zilizotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuhusu program ya uhamiaji wa watu wa Afghanistan. Majimbo mengine ni Alabama na Mississippi kulingana na maafisa wa wizara hiyo.

Hata hivyo majimbo ya Hawaii, South Dakota, West Virginia, Wyoming na Washington DC hayatarajiwi kupokea wakimbizi wowote kwenye kundi la kwanza lililotoroka Afghanistan wakati wa siku za mwisho za kuondoka kwa vikosi vya Marekani mwezi uliopita.

Utawala wa Biden umeliomba bunge kuidhinisha fedha zitakazo saidia kuwapa hifadhi wakimbizi 65,000 kutoka Afghanistan nchini Marekani kufikia mwisho wa mwezi huu, pamoja na wengine 95,000 kufikia September mwakani. Biden amemteua gavana wa jimbo lake la Delaware Jack Markell kuongoza juhudi za kutoa hifadhi kwa wakimbizi kutoka Afghanistan hapa Marekani.

XS
SM
MD
LG