Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:15

Wakenya wazuia magari kuonyesha kero la ongezeko la bei ya mafuta


William Ruto of Kenya
William Ruto of Kenya

Wakenya wameeleza hasira zao Alhamisi kwa kuzuia usafiri wa magari katika sehemu mbali mbali za nchi kutokana na kuongezeka bei za mafuta, ambayo inatishia kuikandamiza jamii ambayo tayari inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kwa sababu ya janga la COVID-19.

Bei za mafuta hivi sasa ziko juu baada ya mamlaka ya kudhibiti nishati nchini wiki hii kusitisha ruzuku kwa ajili ya petroli, dieseli na mafuta ya taa iliyokuwa imeanzishwa mapema mwaka huu ili kuwafariji watu waliokasirishwa na kupanda kwa gharama za maisha.

Makamu wa Rais William Ruto, ambaye yuko katika mzozo wa wazi na Rais Uhuru Kenyatta, amekosoa uamuzi huo, akionya utapelekea kuongezeka kwa gharama za maisha katika kila kitu.

“Ni Kosa kwa hili kufanyika katikati ya janga la COVID-19,” amesema, akiitaka wizara ya nishati na bunge kulitafutia jambo hilo ufumbuzi.

Uchumi huu mkuu wa Afrika Mashariki umeathirika sana kwa kupoteza ajira wakati jumla ya pato la taifa likisinyaa mwaka jana kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo mitatu, huku COVID-19 ikiathiri sekta imara kama utalii.

Kufutwa kwa ruzuku hizo, iliyotekelezwa Jumatano, imeongeza bei ya petroli mjini Nairobi kwa karibu asilimia sita na kufikia takriban shilingi 135 (kama dola 1.20 au euro 1.00) kwa lita.

Na gharama hiyo imepangwa kuongezeka zaidi baada ya kuanzishwa kwa kodi mpya ya asilimia tano ya ushuru wa mafuta kuanzia Octoba 1.

“Kuongezeka kwa bei ya mafuta ni ujinga, inaonyesha namna serikali hii haiku makini na ukweli wa hali za watu, vipi wanataka sisi tuweze kuishi,” amesema James Mwangi, 42, muuza magari yaliyotumika mjini Nairobi.

“Ongezeko la bei ya mafuta inamaanisha kuongezeka kwa bei ya vitu vingi vingine.”

Mercilyne Njeri, 35, ambaye anafanya kazi katika hoteli ya kifahari Nairobi, anasema tayari hivi sasa anajaribu kuishi kwa asilimia 60 ya mshahara wake wa kawaida.

“Serikali hii haiko makini, huwezi kuongeza bei ya mafuta wakati tunakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi iliyoletwa na changamoto za COVID-19.”

XS
SM
MD
LG