Katika zoezi hilo Rais wa Jubaland, Somalia, Ahmed Mohamed Islam alishiriki huku akiwafariji watu waliojeruhiwa.
Watu 33 waliuawa katika shambulio hilo na wengine 56 kujeruhiwa.
Shambulizi hilo lililotokea siku ya Ijumaa na kudumu kwa masaa kumi na mbili lilifanyika katika hoteli maarufu ya Medina iliyoko katika eneo la kusini mwa mji wa bandari wa Kismayu. Al-Shabaab wamedai kuhusika na shambulizi hilo.
Ahmed Mohamed Islan, anayejulikana kama Madobe, Rais wa uongozi wa kimkoa wa Jubbaland, alisema "vikosi vyetu vya ulinzi vimeweza kumaliza shambulio hilo baada ya mapambano ya masaa mengi na madhalimu, na hatimaye kuweza kuwahami watu wengi waliokuwa katika eneo hilo wasiokuwa na hatia.