Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:14

Askari wa Kenya wamejeruhiwa na bomu lililotegwa barabarani wakiwa kwenye doria


Charles Owino aliliambia shirika la habari la Reuters alikuwa akisubiri taarifa juu ya idadi kamili ya vifo. Hakuna mtu yeyote aliyedai kuhusika na shambulizi hilo lakini kundi la waasi la Al-Shabaab kutoka Somalia linafanya mashambulizi mara kwa mara kwa vikosi vya usalama vya Kenya

Msemaji wa polisi Kenya, Charles Owino alieleza kuwa bomu lililotegwa barabarani limelipuka na kupiga gari linalofanya doria karibu na mpaka wa kenya na Somalia siku ya Jumamosi na kuwauwa maafisa polisi kadhaa kati ya 11 waliokuwemo ndani ya gari hilo.

Owino aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba alikuwa akisubiri taarifa juu ya idadi kamili ya vifo. Hakuna mtu yeyote aliyedai kuhusika na shambulizi hilo lakini waasi wenye itikadi kali ya Ki-islam nchini Somalia wanafanya mashambulizi mara kwa mara kwa vikosi vya usalama vya Kenya.

Charles Owino, msemaji wa polisi Kenya
Charles Owino, msemaji wa polisi Kenya

Waasi wa kundi la Al-Shabaab la Somalia walidai kuhusika kwa tukio la Ijumaa la utekeji nyara wa polisi watatu wa Kenya wasiovalia sare kutoka Wajir huko kaskazini-mashariki mwa kenya karibu na mpaka wa Somalia. Wakati huo huo msemaji wa al-Shabaab kwa operesheni za jeshi Abdiasis Abu Musab aliiambia Reuters kwa njia ya simu "jana usiku tumedhibiti kijiji kimoja kinachoitwa Konton katika kaunti ya Wajir. Tuliondoka kwenye kijiji hicho na tuliwachukua polisi watatu wa Kenya".

Vikosi vya jeshi la Kenya vinadhibiti sehemu ya kusini mwa Somalia pamoja na kaunti mbili zinazoshirikiana mpaka tangu mwaka 2011.

XS
SM
MD
LG