Rais alijizuia kufika maeneo yalipotokea mashambulizi hayo katika mji wa Dayton na duka la Walmart katika mji wa El-Paso mahala ambapo watu wenye silaha waliuwa watu 31.
Maeneo yote jana Jumatano yalijaa waandamanaji ambao walipinga Trump kutembelea katika miji hiyo huku wakitoa wito wa kurejeshwa muswada wa kudhibiti bunduki.
Wafuasi wa Trump pia walikuwepo kwenye miji yote hiyo. Katika mji wa El Paso uliopo kwenye mpaka wa Texas mahala ambapo siku nne zilizopita mtu mwenye silaha aliuwa watu 22 na kuwajeruhi zaidi ya darzeni mbili wanasiasa walizungumza kwenye tukio hilo na walimkosoa rais Trump kwa maneno yake yanayowagawa watu.
Mbunge wa chama cha Demokrat, Veronica Escobar ambaye wilaya yake inajumuisha eneo la Walmart mahala shambulizi hilo lilipotokea.
Alisema alikataa mwaliko wa kuongozana na Rais Trump wakati wa ziara yake kwenye mji huo, kwa sababu ya taharuki aliyosababisha Rais kwa jamii na nchi nzima.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.