Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:31

Trump kuzuru Ohio, Texas kuomboleza mauaji ya watu 31


Rais Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari (hawako katika picha) kabla ya kuanza ziara yake Ohio na Texas Jumatano
Rais Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari (hawako katika picha) kabla ya kuanza ziara yake Ohio na Texas Jumatano

Rais wa Marekani Donald Trump yuko safarini kuzuru Dayton, Ohio na El Paso, Texas, Jumatano ikiwa ni ziara ya maombolezo ya mauaji ya watu 31 yaliyotokea wikiendi iliyopita.

Ziara ya Trump katika miji hiyo miwili inakuja huku mjadala ukiendelea kuhusiana na sheria ya umiliki wa bunduki, na kukosolewa kwa matamshi ya Trump kuhusu wahamiaji wasiokuwa na stakabadhi, ambayo yametajwa kuwa matamshi ya ubaguzi wa rangi.

Watetezi wa sheria kali za umuliki wa bunduki, walikutana karibu na White House, wakitaka baraza la senate kupigia kura mswada uliopitishwa na baraza la wawakilishi linalodhibitiwa na Wademokrati, unaotaka watu wanaonunua bunduki, kufanyia ukaguzi wa kina kuhusu historia yao.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Washington, DC.

XS
SM
MD
LG