Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:08

Trump aadhimisha Uhuru wa Marekani kwa utaratibu mpya


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Sherehe za kuadhimisha miaka 243 ya kuzaliwa kwa taifa la Marekani zinamuonekano tofauti mwaka 2019, wakati Rais Trump akipanga utaratibu wake binafsi wa kusheherekea kijeshi siku hiyo, ikiwa ni ziada ya maadhimisho ya kawaida yanayofanyika hivi sasa katika mji mkuu wa Marekani.

Rais wa Marekani ambaye ni mfanyabiashara anapanga kutengeneza utaratibu mpya wa sherehe hizo kwa kujiingiza yeye mwenyewe katika sherehe hizo, akionyesha nguvu za jeshi la Marekani, na kuyahamisha na kuongezea maonyesho maarufu ya urushaji fataki

Trump kulihutubia taifa

Rais Donald Trump amepangiwa kulihutubia taifa katika jukwaa la Kumbukumbu ya Lincoln siku ya uhuru wa Marekani Alhamisi jioni. Sehemu maalum ya wageni muhimu itawekwa katika eneo na tiketi kwa ajili ya kukaa katika jukwaa zitatolewa na White House.

Rais pia ameamrisha Jeshi la Marekani kupeleka magari ya kijeshi, vikiwemo vifaru, kwa ajili ya maonyesho hayo. Amri hiyo ya rais imeleta wasiwasi kuwa uzito wa magari hayo yanaweza kuharibu miundombinu katika eneo la uwanja wa National Mall na maeneo jirani.

Sikukuu ya Julai 4, inaadhimisha siku ambayo Marekani ilitangaza uhuru wake kutoka Uingereza 1776 na kuundwa kwa taifa huru la Marekani.

Maandalizi yanaendelea

Wakati huohuo jiji la Washington, mji mkuu wa Marekani linaendelea kujiandaa kwa shamrashamra hizo.

Sauti na mandhari iliyozoeleka na kila Marekani… Sherehe za Siku ya Uhuru wa Marekani zinazofanyika Bunge la Marekani. Lakini kwa upande mwengine wa viwanja vya National Mall, matayarisho yanaendelea kwa ajili ya maadhimisho mapya ya pili ya Rais Donald Trump kuweza kuwasalimia Wamarekani.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Grucci Fireworks Phil Grucci anasema “ Ni namna Wamarekani wanavyoadhimisha siku hiyo, sawa? Sisi tunataka kufanya kitu kikubwa na kinachovutia.”

Kampuni ya Gucci

Gucci ni moja ya kampuni mbili ambazo zimechangia fataki kwa ajili ya sherehe hizo mchango ambao umetambuliwa na Rais kupitia akaunti yake ya Tweet… ambaye ameahidi kuwepo maadhimisho makubwa ambayo hayajawahi kufanyika ikiwemo kuonyesha vifaru vya kijeshi.

Uwepo wa vifaru vya kijeshi vimepelekea baadhi ya watu kusema kuwa rais anafanya sherehe hizo ni za kijeshi wakati zinatakiwa zisiegemee upande wa chama chochote kama sikukuu ya kitaifa. Lakini wako baadhi ya watu ambao wanasema hawajali…

“Ninafahari na nashukuru kwa wale waliotumikia nchi yetu na tunaridhishwa na yale yote waliofanya na familia zao na tunamshukuru rais wetu, anayetambua mchango wao na kuwa na nia ya kuadhimisha hilo,” mtalii Brent Hoban ameeleza.

Chanzo cha fedha za sherehe

Lakini taarifa za sherehe anazoandaa Trump zitalipwa kwa kutumia sehemu ya fedha zilizotolewa kutoka maeneo ya bustani za taifa za Marekani, zinawatia wasiwasi Wademokrat ambao ni Wabunge ambao wanasema fedha hizo hazitakiwi kutumika kwa ajili ya kile kinachoonekana kuwa ni mkutano wa kisiasa wa rais.

Mshauri wa White House Kellyanne Conway ameelekeza maswali juu ya gharama waulizwe Wizara ya Ulinzi wakati akiwa anagusia hotuba ya rais…

Mshauri wa White House

Mshauri wa White House Conway anasema :”Demokrasia yetu adhimu na wito kwa uzalendo wetu, mafanikio ya uongozi huu wa kuweza kuleta ajira nyingi kwa watu wetu, na nini tulichofanya kwa wastaafu wetu waliopigana vita.”

Hotuba hiyo pamoja na sherehe zote mbili za kurusha fataki zinaweza kuwa mashaka. Hali ya mvua zenye upepo mkali imetabiriwa kuwepo Washington, DC, wakati wa joini wa sikukuu hiyo.

XS
SM
MD
LG