Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:21

Je, mitandao ya kijamii iwajibishwe kwa kuchapisha habari feki?


Mwananchi wa India akifanya uhakiki kupitia akaunti ya twitter ya kampuni ya Alt News, Tovuti yenye kusaidia kutambua habari feki , huko New Delhi, India, Aprili 2, 2019.
Mwananchi wa India akifanya uhakiki kupitia akaunti ya twitter ya kampuni ya Alt News, Tovuti yenye kusaidia kutambua habari feki , huko New Delhi, India, Aprili 2, 2019.

Wakati Kanisa Katoliki la Notre Dame liliposhika moto, habari iliyokuwa ikienezwa kupitia mtandao wa Facebook – picha ya video ikionyesha mtu aliyevaa mavazi ya Kiislam, iliyokuwa haionyeshi vizuri, akiwa ndani ya kanisa.

Wahakiki wa habari duniani kuthibisha ukweli wake walichukuwa hatua na kuonyesha kuwa video hiyo na uwekaji wa picha hiyo ulikuwa ni uzushi na hivyo posti hiyo haikupata umaarufu wowote.

Lakini wiki hii, serikali ya Sri Lanka kwa kipindi kifupi ilifunga mtandao wa Facebook na majukwaa mengine kuzuia kuenea kwa habari za upotoshaji wakati wa tukio la shambulizi la mabomu Jumapili ya Pasaka nchini humo yaliouwa watu 250.

Mwaka 2018, habari za upotoshaji katika mtandao wa Facebook zililaumiwa kwa kusababisha ghasia nchini humo.

Mitandao ya Facebook, Twitter, Youtube na mengine imeendelea kulaumiwa kuhusika na maudhui katika majukwaa yao wakati dunia ikijaribu kukabiliana na uhalisia wa mambo yanapokuwa yanatokea.

Kuanzia watungaji sheria mpaka umma wote, kumekuwa na ongezeko la kilio dhidi ya majukwaa haya ya mitandao ya kijamii juu ya habari za upotoshaji hasa pale zinapokuwa zinavilenga baadhi ya vikundi.

Kwa miaka mingi, baadhi ya wakosoaji wa makampuni ya mitandao ya kijamii, ikiwemo Twitter, Youtube na Facebook, wamewatuhumu kuchukuwa hatua isiyoridhisha katika kufuatilia na kuondoa habari zenye kupotosha kutoka katika majukwaa yao.

Juu ya yote, majukwaa ya intaneti kwa ujumla hayana jukumu la kisheria kwa maudhui yanayowekwa kwenye mitandao hiyo, Ni shukrani kuwa sheria ya serikali kuu ya Marekani ya 1996 inayosema kuwa wao siyo wachapishaji. Sheria hii imetumika kama ni kinga kwa uhuru wa kujielezea katika mitandao.

Na kuwa kinga hiyo ya kisheria imekuwa ni chachu ya ongezeko kubwa la makampuni ya Internet. Lakini kunaongezeko la kukubaliana kuwa makampuni yanajukumu la kimaadili kwa maudhui yoyote yanayopotosha jamii, na hasa iwapo maudhui hayo yanawafuatiliaji na imekusudiwa kuyalenga makundi fulani.

Katika mahojiano yaliofanywa hivi karibuni na Kamati ya Sheria ya Baraza la Wawakilishi juu ya wazungu wenye misimamo ya ubaguzi na jinai ya chuki dhidi ya makundi mengine, Mwakilishi Sylvia Garcia, Mdemokrat kutoka Texas, aliwahoji wawakilishi wa Facebook na Google juu ya sera zao.

“Mmechukua hatua gani kuhakikisha kuwa watu wenu wote duniani wanafahamu ujumbe wenye jinai unaokusudiwa kuwafikia kikundi fulani, wanajua maneno muhimu, namna yalivyoelezewa, vitu ambavyo watu wanavijibu, ilituweza kuwa tunakabiliana na kuchukua tahadhari mapema kuzuia baadhi ya lugha hii?" anasema Garcia.

Facebook, ambayo pengine inahesabiwa zaidi na umma kuwa na habari za uongo, haitosema kuwa ni kampuni ya habari.

Lakini imechukuwa kidogo jukumu la kusimamia maudhui inayowekwa katika jukwaa lake, amesema Daniel Funke, mwandishi wa mtandao wa kimataifa wa kuhakiki habari iwapo ni za kweli katika Chuo cha Poynter.

Mtandao huo wa kijamii mkubwa unatumia mkusanyiko wa teknolojia na binadamu kuzuia habari za uongo na ujumbe wa namna hiyo ambao unayalenga baadhi ya makundi.

Inashirikiana na wahakiki wengine wanaopima ukweli wa taarifa zinazotolewa ili kuondoa maudhui yasiokubalika na imeajiri maelfu ya watu kupambana na maudhui potofu katika jukwaa lake.

XS
SM
MD
LG