Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:36

Shambulizi la Msikitini New Zealand : Uchunguzi wa awali unaonyesha mshambuliaji ni "gaidi mwenye mrengo wa kulia"


Picha inaonyesha mshambuliaji aliyetumia bunduki alipokuwa anaingia msikitini kufanya mashambulizi katika mji wa Christchurch, New Zealand, Machi 15, 2019.
Picha inaonyesha mshambuliaji aliyetumia bunduki alipokuwa anaingia msikitini kufanya mashambulizi katika mji wa Christchurch, New Zealand, Machi 15, 2019.

Watu wasiyopungua 49 wameuawa na zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya sana Ijumaa katika shambulizi lililofanyika katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch, New Zealand.

Wanaume watatu na mwanamke mmoja wanazuiliwa na polisi. Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amesema hakuna kati yao aliyekuwa katika orodha ya watu hatari wanaofuatiliwa na vyombo vya usalama.

Mwanaume mwenye umri wa miaka 28 amefunguliwa mashtaka ya mauaji. Anatarajiwa kupelekwa mahakamani Jumamosi, kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Mike Bush.

Wakati Bush alikataa kutaja jina la mtu huyo aliyefunguliwa mashtaka, kituo cha Televisheni cha New Zealand (TVNZ) kimemtaja mtu huyo aliyetumia bunduki kuwa ni Brenton Tarrant, 28, kutoka Grafton, New South Wales, Australia. Maafisa nchini Australia wamethibitisha kuwa mtu huyu aliyetumia silaha hiyo ni raia wa Australia.

Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison amesema mtu huyo aliyewekwa chini ya ulinzi wa polisi ni raia wa Australia. Morrison amesema mshukiwa huyo aliyefanya shambulizi ni “gaidi mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia.”

Kamishna Bush amesema sehemu ya uchunguzi huo utakuwa kuangalia nyuma kila kinachowezekana kuhakikisha kuwa sisi katika vyombo vya kusimamia sheria na uslama, hatutapoteza fursa yeyote kuzuia kitendo hiki cha kinyama kutokea tena.”

Walionusurika katika shambulizi hilo wamesema kuwa walioweza kukimbia kuokoa maisha yao, na walipokuwa katika harakati hizo walishuhudia watu wakiwa wameanguka wanavuja damu katika eneo hilo la msikiti wa Al- Noor.

Polisi wamewataka watu wa eneo hilo kuchukuwa tahadhari wakisema kuwa hali bado ni tete na tayari wameweza kuharibu vilipuzi vilivyokuwa vimetegwa katika eneo hilo.

Misikiti hiyo miwili ilishambuliwa wakati wa sala ya Ijumaa iliyohudhuriwa na mamia ya waumini.

Mshambuliaji huyo aliyetumia bunduki alikuwa anaonyesha shambulizi hilo alilolifanya mubashara katika Facebook kupitia kamera aliyokuwa ameivaa kichwani, na picha zilionyesha jinsi wahanga wa mauaji hayo walivyokuwa wanauawa katika msikiti huo. Mshambuliaji huyo alionyesha shambulizi hilo baada ya kuchapisha msimamo wake ambapo amewaita wahamiaji ni “wavamizi”. Mitandao ya jamii iliamrishwa mara moja kuondoa picha hizo za mauaji ya kinyama.

Watu 41 kati ya wale waliouawa walikuwa katika msikiti mmoja na watato ni kati ya watu 48 wanaopatiwa matibabu kutokana na majeraha ya risasi, maafisa wamesema.

XS
SM
MD
LG