Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:16

Tillerson ashtushwa na ripoti za mauaji Rohingya


Waislam wa Rohingya wakisafiri kwenye mashua iliyotengenezwa kwa plastiki kuvuka mto Naf kuelekea Bangladesh wakikimbia mauaji Jumapili Novemba 12, 2017.
Waislam wa Rohingya wakisafiri kwenye mashua iliyotengenezwa kwa plastiki kuvuka mto Naf kuelekea Bangladesh wakikimbia mauaji Jumapili Novemba 12, 2017.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson, wakati wa ziara yake huko Myanmar ameshtushwa na “ripoti za kuaminika zinazohusu kuenea mauaji yanayofanywa na vikosi vya usalama na makundi ya ulinzi ya nchi hiyo."

Kutokana na mauaji hayo yanayodaiwa kufanywa na serikali ya Myanmar katika jimbo la Rakhine, Tillerson amesema “vikwazo vya uchumi kwa maana pana zaidi” dhidi ya nchi hiyo havitakuwa ni shauri la busara.

“Nina wakati mgumu kuangalia vipi vikwazo hivyo vitaweza kutatua mgogoro huu,” amesema Tillerson, akieleza kile Umoja wa Mataifa walichokiita “ni mpango ulioandaliwa wa mauaji ya kikabila” ya Waislam walio wachache wa Rohingya.

Ameongeza kuwa vikwazo vilivyokuwa vimeelekezwa kwa watu binafsi “inaweza ikawa ni hatua sahihi.” Alikuwa akizungumza akiwa pamoja na kiongozi anayetambuliwa wa Myanmar Aung San Suu Kyi.

“Tunataka kuiona Myanmar inafanikiwa,” amesema, akitangaza kuwa Marekani itatoa dola milioni 47 zaidi za misaada kwa wakimbizi wa Rohingya, ikiwa ni jumla ya kiasi cha dola milioni 87 mwaka huu.

Tillerson amesema matukio katika eneo hilo lenye mgogoro la jimbo la Rakhine “ni la kinyama” na ameihimiza Myanmar kutekeleza mapendekezo ya ripoti iliyoandaliwa chini ya uongozi wa Katibu Mkuu mstaafu wa UN Kofi Annan, ambayo imehusisha kuweka utaratibu wa kuwawezesha watu wa Rohingya kupata uraia kamili.

Ann San Suu Kyi alijibu kwa kumshukuru Tillerson kwa kukubali kuwepo changamoto na kuwa tayari kupokea ushauri. “Ni nadra kuwepo watu waliotayari kupokea ushauri,” amesema.

Mara baada ya kuwasili katika mji mkuu Naypyidaw Jumatano, Tillerson alikutana na Mkuu wa Majeshi Min Aung Hlaing, ambaye majeshi yake yametuhumiwa kwa kuanzisha kampeni ya kuaangamiza kabisa vijiji vya Rohingya huko kaskazini magharibi ya Jimbo la Rakhine kwa kujibu mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya vituo vya polisi na vikosi vya waasi wa Rohingya mwezi August.

Kampeni hiyo ya kijeshi ilipelekea wimbi kubwa la wakimbizi 600,000 wa Rohingya kuingia nchi ya jirani ya Bangladesh, ambao wameviambia vikundi vya haki za binadamu kuwepo mauaji ya kinyama yanayofanywa na vikosi vya usalama vya serikali, ikiwemo kupigwa risasi watu ovyo, vitendo vya ubakaji na uchomaji wa nyumba katika vijiji vyao.

Maafisa wa Jeshi la Myanmar wamesema kuwa uchunguzi wa ndani umegundua kuwa hakuna ushahidi kuwa askari hao walitenda mauaji hayo dhidi ya watu wa Rohingya na kuwa vikosi hivyo viliuwa tu “magaidi” wa Rohingya 376 wakati wakipambana nao.

Ripoti hiyo ya jeshi la Myanmar imetupiliwa mbali na Kikundi kinachosimamia haki za binadamu chenye makao yake New York kuwa ni jaribio la jeshi hilo “kujikosha” kutokana na vitendo vyao.

XS
SM
MD
LG