Waislamu ambao ni asilimia 10 ya wakazi milioni 21 wa Sri Lanka. Wananchi wa Sri Lanka waliowengi ni kabila la Sinhale wanaofuata dini ya kibuda.
Makamu wa rais wa Baraza la Waislamu wa Sri Lanka amesema tayari wameshuhudia baadhi ya watu wakirusha mawe kwenye misikiti mbali mbali, huku watu wengine wakihama makazi yao kutokana na hofu ya kushambuliwa.
Wakati huohuo Waziri wa Ulinzi wa Sri Lanka anasema idadi ya waliofariki imeongezeka na kufikia 359, na kumetokea mlipuko mmoja wa bomu Jumatano, karibu na jengo la sinema la Savoy, na bomu jingine kupatikana katika mtaa wa biashara wa Colombo.
Katika tukio hilo jipya la mlipuko hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa. Maafisa wa usalama wanasema watu 60 wamekamatwa hadi hivi sasa ili kuhojiwa kutokana na mashambulio hayo ya Jumapili.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.