Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 08:38

New Zealand kupiga marufuku bunduki rashasha


Waziri mkuu wa New Zealand, Jacinda Arden
Waziri mkuu wa New Zealand, Jacinda Arden

Waziri mkuu wa New Zealand, Jacinda Arden, alitangaza Alhamisi kwamba utawala wake utapiga marufuku silaha zote zinazofanana na zile za kijeshi, ikiwa ni pamoja na bunduki rashasha, kufuatia mashambulizi yaliyopelekea vifo vya watu 50 Ijumaa wiki jana.

Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari mjini Wellington, Arden alisema mswada wa kupiga marufuku silaha zinazofanana na zile zilizotumika katika mashambulizi hayo mjini Christchurch utawasilishwa bungeni haraka kama hatua ya dharura.

Wabunge walisema Jumatatu kwamba wataunga mkono hatua hiyo.

Haya yalijiri huku rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akisema kwamba Ukristo haufai kulaumiwa kwa mauaji hayo yaliyotekelezwa wiki jana katika misikiti miwili tofauti.

Erdogan alisema mshambuliaji huyo si tofauti na magaidi wa Islamic State.

Katika Makala ya maoni binafsi yaliyochapisha kwenye gazeti la The Washington Post, mwanasiasa huyo ambaye ni muumini wa dini ya Kiislamu, alipinga vikali dhana kwamba mshambuliaji huyo alikuwa anafuata mafunzo ya dini ya Kikristo. Alisema kilichotokea nchini New Zealand kilisababishwa na chuki na kukosa ufahamu.

Mamlaka nchini New Zealand zimesema kwamba Brenton Tarrant, ambaye anashukiwa kutekeleza mashambulizi hayo, huenda alifuatilia kwa karibu vita vya kiitikadi, ambavyo vina historia ndefu kati ya Uislamu na Ukristo.

Erdogan alizitaka nchi za magharibi kukemea ubaguzi wa kila aina na chuki ambayo imeongezeka katika maeneo mbalimbali ulimwenguni katika miaka ya karibuni.

XS
SM
MD
LG