Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:39

Kuhusu Sauti ya Amerika (VOA)


Sauti ya Amerika (VOA) ni taasisi kubwa yenye aina mbalimbali za majukwaa ya matangazo ya habari za kimataifa, inayoandaa maudhui katika lugha zaidi ya 45 kwa wasikilizaji wenye kukabiliwa na ufinyu wa kupata habari au hawana njia ya kupata habari kutoka vyombo vilivyo huru.

Tangu ilipoanzishwa mwaka 1942, VOA imejizatiti kutoa matangazo kamilifu, huru na kuwaeleza wasikilizaji wake ukweli. VOA inafadhiliwa kikamilifu na walipa kodi wa Marekani ikiwa ni sehemu ya Taasisi ya Habari ya Kimataifa ya Marekani (USAGM).

Jukumu la VOA na uhuru wa habari uliowekwa na sheria inayowalinda waandishi wa habari wa VOA dhidi ya ushawishi, shinikizo, au kulipiziwa kisasi kunakoweza kufanywa na maafisa wa serikali au wanasiasa.

Mwaka 1976, Rais Gerald R. Ford alisaini Mkataba wa VOA, unaoeleza kuwa :

VOA itajishughulisha bila ya kusita kuendelea kuwa ni chanzo cha habari chenye kutegemewa na kuaminika. Habari zinazotolewa na VOA zitakuwa sahihi, zisizo na upendeleo na kamili.

VOA itaiwakilisha Marekani, na siyo kikundi kimoja cha jamii ya Marekani, na hivyo kutoa muelekeo wenye uwiano na ukamilifu wa fikra muhimu za Marekani na taasisi zake.

VOA itatoa sera za Marekani kwa ufasaha na ubora wake, na itaandaa mijadala makini na maoni juu ya sera hizi.

Mnamo mwaka 1994, Bunge la Marekani lilipitisha Sheria ya matangazo ya kimataifa ya Marekani. Sheria hii pia inataka kazi za waandishi wa habari ziwe za kuaminika, sahihi, zisizo kandamiza upande wowote.

Mwaka 2016, Bunge la Marekani kwa mara nyengine liliingiza katika sheria ya kuidhinisha Ulinzi wa Taifa kuwa ukusanyaji wa habari na majukumu ya kupasha habari lazima yaendelee kuwa huru na yasiyokandamiza upande wowote.

Kila siku, waandishi wa VOA wanafanya kazi kwa bidii kuweka mfano bora wa misingi ya uhuru wa habari ulimwenguni.

VOA

XS
SM
MD
LG