Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 00:33

Trump aagiza maomboleza ya kitaifa kwa wahanga wa Texas, Ohio


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump Jumapili ameamrisha bendera zote za taifa zipandishwe nusu mlingoti katika afisi zote za serikali katika kipindi cha siku 5, ili kutoa heshma kwa wahanga wa mashambulizi ya bunduki yaliotokea mwishoni mwa juma mijini El Paso katika jimbo la Texas na Dayton katika jimbo la Ohio.

Mashambulizi hayo mawili yaliuua watu 29. Rais Trump ametaja mashambulizi hayo kuwa yanatokana na matatizo ya maradhi ya akili. Trump atatoa taarifa rasmi Jumatatu kuhusu mashambulizi hayo.

Trump amewaambia waandishi wa habari kuwa chuki haina nafasi nchini Marekani, na kwamba juhudi zinafanyika ili kuzuia mashambulizi mengine yasitokee siku za usoni.

Viongozi wa jimbo la Texas wamesema shambulizi la El Paso ni ugaidi wa ndani, na waendesha mashtaka wanapanga kuomba adhabu ya kifo dhidi ya mshukiwa wa shambulizi hilo.

Wagombea wengi wa kiti cha urais katika chama cha Demokrati wamemshtumu rais Trump kwa kile wanachosema matamshi yake ya chuki dhidi ya wahamiaji ndio yamechochea shambulizi lililotokea mji wa El Paso.

Rais wa Mexico Manuel Lopez Obrador amethibitisha kuwa raia 6 wa Mexico ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulizi lililofanyika ndani ya duka la Walmart katika mji huo wa El Paso ambao unapakana na Mexico.

Mashambulizi ya El Paso na Dayton ni ya 21 na 22 kufanyika tangu mwaka 2019 ulipoanza.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG