Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 15:09

12 wauawa katika shambulizi la risasi Virginia Beach, Marekani


Eneo kulikotokea shambulizi mjini Virginia Beach, Virginia nchini Marekani.
Eneo kulikotokea shambulizi mjini Virginia Beach, Virginia nchini Marekani.

Polisi wa jimbo la Virginia nchini Marekani walisema Ijumaa jioni kwamba watu 12 waliuawa katika shambulizi la risasi  mjini Virginia Beach huku wengine sita, akiwemo afisa wa polisi, wakipata majeraha mabaya na kulazwa hospitalini.

Walioshuhudia kisa hicho walisema kuwa mtu aliyejihami na silaha nzito, ikiwemo bunduki ya rashasha, alivamia jengo la manispaa kwenye mji huo na kuanza kufyatua risasi kiholela.

Mamlaka zilisema mshambuliaji huyo aliingia kwenye maosisi kadhaa akifyatua risasi.

Kwa mujibu wa polisi wa mji huo, mshambuliaji huyo alikuwa mfanyakazi kwenye jengo hilo ambalo ni la ghorofa tatu.

Akihutubia waandishi wa habari baada ya mkasa huo, Meya wa mji wa Virginia Beach, Bobby, Dyer, alisema kwamba wengi wa waliouawa walikuwa wakazi wa mji huo.

"Huu ndio mkasa mkubwa zaidi katika historia ya Virginia Beach. Waliouawa na kujeruhiwa ni marafiki, majirani zetu na wafanyakazi wenzetu," alisema Meya Dyer.

Mkuu wa polisi Jim Cervera aliwaambia waandishi wa habari kwamba mshambuliaji aliuawa wakati wa makabiliano na polisi.

Hilo ndilo shambulizi la hivi karibuni kabisa nchini Marekani ambapo mshambuliaji alitumia silaha nzito ambazo kwa kawaida hutumiwa na wanajeshi katika mazingira ya kivita.

Suala hilo limekuwa likiibua mjadala mkubwa kuhusu iwapo ni jambo la busara kwa raia kukubaliwa kumiliki silaha kama hizo.

Kwa ujumla wanasiasa wa mirengo miwili mikubwa ya Marekani - Warepublikan na Wademoktat wamekuwa na misimamo inayohitilafiana kuhusu suala hilo.

Habari zaidi zitafuata....

XS
SM
MD
LG