Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:09

Shambulizi Indonesia lauwa 11, kujeruhi 41


Rais akizuru eneo la tukio la kujitoa muhanga huko Surabaya, lililotokea mapema Jumapili, Mei 13, 2018.
Rais akizuru eneo la tukio la kujitoa muhanga huko Surabaya, lililotokea mapema Jumapili, Mei 13, 2018.

Polisi nchini Indonesia wanasema familia moja yenye vijana na watoto, ndio waliokuwa nyuma ya shambulizi la kujitoa muhanga katika makanisa matatu Jumapili ambalo limeuwa sio chini ya watu 11 na kujeruhi wengine 41 katika mji wa Surabaya.

Kikundi cha Islamic State kimedai kuhusika na shambulizi hilo la mabomu katika mji huu wa pili kwa ukubwa nchini Indonesia.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari Rais wa Indonesia Jokowi Widodo anatembelea eneo moja ambalo shambulizi hilo la bomu lilitokea huko Surabaya

Mkuu wa Polisi wa Taifa Tito Karnavian amesema wajitoa muhanga hao ni pamoja na mama na baba wa familia hiyo, mabinti wao wawili kati ya miaka 9-12 na wavulana wawili wa familia hiyo. Watu hawa wote wanadaiwa kuwa na mahusiano na kikundi cha Islamic State cha Jemaah Ansharut Daula kilichowahamasisha.

Jumuiya za Kiislam na Kikristo nchini Indonesia zimelaani mashambulizi hayo na kutoa tamko la pamoja likisema hakuna “hata dini moja duniani ambayo inahalalisha vitendo vya uvunjifu wa amani katika kufikia malengo yake.” Jumuiya hizo zimeitaka serikali kuchukua hatua madhubuti na za haraka” kukabiliana na ugaidi na misimamo mikali.

Polisi wameamrisha makanisa yote kufungwa kwa muda katika mji wa Surabaya. Pia sherehe za karamu kubwa katika mji pia zimesimamishwa.

Makanisa huko mji mkuu wa Indonesia,Jakarta yamesitisha ibada za asubuhi. Jakarta iko katika ulinzi mkali baada ya mashambulizi hayo ya mabomu matatu huko Surabaya. Jeshi la Polisi la taifa wameongeza ulinzi kote katika mji huo, hasa kuzunguka vitu muhimu na maeneo ya mikakati.

Hakuna maelezo zaidi juu ya sababu zilizopelekea polisi kuongeza ulinzi mkali, au kuwa kuna tishio lolote jengine limetolewa la shambulizi la kigaidi dhidi ya mji huo mkuu.

Mashambulizi hayo katika mji wenye Waislam wengi Indonesia yamekuja masiku kadhaa baada ya polisi kumaliza vurugu na utekaji katika jela moja karibu na Jakarta ambapo maafisa sita waliuwawa na mfungwa moja walipoteza maisha.

XS
SM
MD
LG