Donald Trump na Joe Biden wanaingia katika mdahalo wao wa kwanza katika kampeni hii kila mmoja akiwaambia wapiga kura kwamba kumchagua mpinzani wake itakuwa ni janga.
Trump anasema Biden anaiharibu nchi.
Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican: “Mfumuko wa bei unazidi kuongezeka. Uhalifu haudhibitiwi. Ulaya iko katika vurugu, Mashariki ya kati inalipuka. Iran imekuwa jasiri. China inafanya mambo yake. Na hii ni mbaya sana, rais mbaya anatusukuma kuelekea kwenye Vita vya Tatu vya Dunia.”
Biden anasema Trump atairudisha nchi nyuma.
Rais wa Marekani Joe Biden, anasema: “Maendeleo yote, uhuru, furs azote ziko katika hatari. Trump anajaribu kuifanya nchi isahau jinsi tulivyokuwa gizani na mambo ambayo hayakuwa yamekaa vyema wakati alipokuwa rais. Hatutasahau kamwe.”
Ukusanyaji maoni ya umma unaonyesha kuwa ushindani wa karibu sana, kuongeza mtazamo kwa mdahalo huu, anasema profesa Alan Schroeder wa masuala ya uandishi wa habari katika chuo kikuu cha Northeastern.
Alan Schroeder, Chuo Kikuu cha Northeastern anasema: “Nadhani hiyo inaweka aina fulani ya shinikizo kwa wagombea wote wawili, kote katika misingi ya fursa ambazo zinajitokeza kwao katika mdahalo. Lakini pia kuna athari.”
Mdahalo wa Aina Yake
Huu ni mdahalo wa aina yake ukiwajumuisha wagombea wote akiwa ni rais ambaye yuko madarakani na rais wa zamani, anasema Kathleen Hall Jamieson profesa wa mawasiliano katika chuo kikuu cha Pennsylvania.
Kathleen Hall Jamieson, Chuo Kikuu cha Pennsylvania anaeleza: “Kwahiyo, umma una uwelevu zaidi kuhusu wagombea wote hawa wawili kama watu binafsi, wanawafahamu tabia zao, mawazo yao, na fikra zao. Lakini mwaka huu, kwasababu ya umri kwa wote, kuna haja, hata kama unadhani unafahamu mengi kuhusu wagombea wote wawili – na una fursa nzuri mwaka huu kwa kuwa na uwezo wa kusema, kiakili je wanatosha kuwa rais wa Marekani na ki akili ni thabiti vya kutosha kuwa rais wa Marekani?”
Ujumbe wa Muda
Midahalo ya kisiasa ni kuhusu ujumbe na muda, anasema mchambuzi wa siasa Brett o”Donnell.
Brett O’Donnell, O’Donnell & Associates anaeleza:
“Lazima upeleke ujumbe mara kwa mara katika mdahalo, lakini pia unataka kuwa na muda fulani kwenye mdahalo ambao utaonyesha kung’aa kwa kusema kile ambacho waandishi watakitupia jicho ambacho kitakufanya uonyeshe ushindani wako.”
Huu utakuwa mdahalo wa mapema sana wa urais katika historia ya Mareakni, si Trump wala Biden ambaye ameteuliwa rasmi kama mgombea wa chama. Hakutakuwa na maelezo ya ufunguzi leo usiku. Wagombea wote wawili microphone zao zitazimwa wakati siyo zao yao kuongea.