John Bolton amesema Jumapili, wakati akizuru Israeli, kuondoka kwa majeshi ya Marekani kutafungamana na kulitokomeza kwanza kundi la Islamic State.
Bolton amesema Trump “anataka khalifa wa ISIS auwawe.”
Mshauri huyo wa usalama amesema pia Marekani inataka Uturuki iwahakikishie usalama wa wapiganaji wa Kikurdi wenye mafungamano na Marekani kabla ya majeshi yake kuondoka Syria.
Trump alikuwa amekosolewa wakati alipotangaza kuwa majeshi ya Marekani yataondoka Syria ambako kungefanyika ndani ya wiki mbili.
Kauli ya Bolton ni uthibitisho wa mara ya kwanza kwa umma kuwa mchakato wa kuondolewa majeshi ya Marekani umecheleweshwa.