Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:01

Bolton aionya Syria juu ya matumizi ya silaha za kemikali


Mshauri wa Usalama wa Taifa John
Bolton
Mshauri wa Usalama wa Taifa John Bolton

Mshauri wa Usalama wa Taifa wa John Bolton ameionya serikali ya Syria isidhani kuwa hatua inayosubiriwa ya kuondosha majeshi kutoka nchini humo kama ni ruhsa ya wao sasa kutumia silaha za kemikali.

“Hakuna kabisa mabadiliko juu ya msimamo wa Marekani dhidi ya matumizi ya silaha za kemikali zinazo tumiwa na utawala wa Syria na hakuna mabadiliko kabisa juu ya msimamo wetu kwamba matumizi yoyote ya silaha za kemikali yatakabiliwa na hatua kali sana, kama tulivyokuwa tumefanya mara mbili hapo awali,” Bolton aliwaambia waandishi akiwa katika ndege yake muda mfupi kabla ya kutua Tel Aviv Israel.

Kwa hiyo utawala huo, utawala wa Assad usijidanganye juu ya suala hilo.”

Bolton aliongeza : “ Wakati tukifafanua jinsi utaratibu wa kuondoa majeshi utakavyo kuwa na mazingira yake, hatutaki utawala wa Assad kuangalia hatua hii kuwa inapunguza shinikizo letu dhidi ya matumizi ya silaha za maangamizi ya umma.”

XS
SM
MD
LG