Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 19:48

Juhudi za kidiplomasia kati ya Ankara na Washington zinaendelea


Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump

Wachambuzi wanaonya kuna ujumbe mchanganyiko kati ya washirika wawili wa NATO katika kuzuia juhudi hizo. YPG ni mshirika muhimu katika vita vya Washington dhidi ya kundi la Islamic State

Juhudi za kidiplomasia zinaendelea kuepuka mgogoro kati ya Ankara na Washington kuhusu tishio la mashambulizi ya Uturuki dhidi ya vikosi vya kikurdi nchini Syria vinavyoungwa mkono na Marekani. Lakini wachambuzi wanaonya kuna ujumbe mchanganyiko kati ya washirika wawili wa NATO katika kuzuia juhudi hizo.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alizungumza na waandishi wa habari Jumatau alitangaza Rais wa Marekani Donald Trump alijibu kwa matumaini kufanyika kwa mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa kikurdi wa Syria-YPG.Ankara inawashutumu YPG kushirikiana na kundi la waasi la PKK la Kikurdi ambalo limekuwa likifanya uwasi kwa miongo kadhaa nchini Uturuki.

Siku ya Jumatatu balozi wa Marekani kwa masuala ya Syria Jim Jeffrey alionekana kupingana na Erdogan. Jeffery alisema “tunafikiri kwamba kila mapigano huko kaskazini-mashariki mwa Syria kwa mtu yeyote ni wazo baya na huo ulikuwa msimamo ambao niliuelezea nilipokuwa Ankara kwa kila mtu kuanzia kwa Rais kwenda chini.

YPG ni mshirika muhimu katika vita vya Washington dhidi ya kundi la Islamic State. Takribani wanajeshi 2,000 wa Marekani wako na wamangambo katika eneo ambao lililengwa na Ankara. Erdogan alisema wanamgambo wa Kikurdi wataondolewa kutoka mto Euphrates kwenye mpaka wa Iraq.

XS
SM
MD
LG