Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:32

Marekani inatathmini tena sera zake kwa Afrika


John Bolton, mshauri wa usalama wa taifa Marekani, Dec. 13, 2018.
John Bolton, mshauri wa usalama wa taifa Marekani, Dec. 13, 2018.

Mshauri wa usalama wa taifa Marekani alisema mabadiliko ya sera pia yanamaanisha kukabiliana haraka na kuongezeka kwa ushawishi wa kifedha na kisiasa wa China na Russia barani Afrika

Marekani inaanzisha haraka sera mpya kwa Afrika. maelezo zaidi yalitolewa Alhamisi katika hotuba ya mshauri wa rais wa usalama wa taifa, John Bolton.

Misaada yote ya Marekani kwenda Afrika ambayo ni jumla ya dola bilioni 8 katika kila mwaka wa fedha kwa vipindi viwili vilivyopita inafanyiwa tathmini ya mwisho kwa mujibu wa Bolton.“Kulingana na mtazamo wetu mpya, kila uamuzi tunaofanya, kila sera tunayofuata na kila dola ya msaada tunayotumia itakuwa kipaumbele cha Marekani katika eneo”.

Katika hotuba yake mshauri huyo wa usalama wa taifa alisema mabadiliko ya sera pia yanamaanisha kukabiliana haraka na kuongezeka kwa ushawishi wa kifedha na kisiasa wa China na Russia barani Afrika.

Wakati Bolton alipozungumzia sera ya utawala kwa Afrika, waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis yeye alitangaza kuwa Marekani hivi sasa kamwe haitasaidia tume za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa ambazo hazionyeshi maendelezo na mafanikio na wala haziwajibiki.

Jim Mattis, waziri wa ulinzi wa Marekani
Jim Mattis, waziri wa ulinzi wa Marekani

Mattis alisema hakuna uhalali kwa tume ambazo zinapewa fedha nyingi na badala yake hupeleka wanajeshi ambao wana vifaa duni na hawatoi ulinzi unaostahili kwa jamii ambazo ziko katika mazingira hatari huko wanakofanya ulinzi wa amani.

Marekani ni mfadhili mkubwa wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa ambapo inatoa takribani theluthi moja ya bajeti yake ya dola bilioni 6.7 kwa mwaka wa fedha ulioanza Julai mosi 2018 hadi June 30 mwaka 2019. Mwaka jana balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley aliongoza juhudi za utawala kupunguza bajeti nzima ya ulinzi wa amani, ambapo Umoja wa Mataifa ulikubali kupunguza bajeti hiyo kwa dola milioni 500.

Pentagon imekuwa ikifanya tathmini tena ya uwepo wa wanajeshi wake na operesheni zake barani Afrika tangu uvamizi uliofanywa nchini Niger mwaka jana na kusababisha vifo vya wanajeshi wanne wa Marekani, wanne wa Nigeria na mfasiri wa kinigeria.

Marekani ina kikosi kidogo katika tume ya kimataifa ya ulinzi wa amani nchini Mali- MINUSMA inachangia chini ya darzeni mbili ya wanajeshi kwa jeshi ambalo lina zaidi ya wanajeshi 13,000 wengi wao kutoka Burkina Faso, Chad, Bangladesh na Senegal.

Baadhi ya wachambuzi wanaonya dhidi ya Washington kuliangalia Bara hilo katika mtazamo huu wakisema itadumaza thamini za kimarekani kwa kuyaangalia tu mataifa ya Afrika kupitia mtizamo wa ushindani.

XS
SM
MD
LG