Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:27

Trump arejea kutoka Iraq, kuendelea kukabiliana na mzozo wa bajeti


Rais Donald Trump na mkewe Melania akipiga picha ya pamoja na wanajeshi wa Marekani nchini Iraq wakati wa ziara yake nchini humo.
Rais Donald Trump na mkewe Melania akipiga picha ya pamoja na wanajeshi wa Marekani nchini Iraq wakati wa ziara yake nchini humo.

Rais Donald Trump wa Marekani amerejea mjini Washington Alhamisi asubuhi ili kuendelea kukabiliana na mzozo wa bajeti uliosababisha serikali kuu kufungwa kwa siku ya sita hivi leo.

Katika ziara yake ya kushitukiza nchini Irak ikiwa ni ya kwanza katika eneo lenye vita kwa kipindi cha miaka miwili ya utawala wake, aliwatembelea wanajeshi wa Martekani katika kambi ya jeshi la anga la Al Asad magharibi ya mji wa Baghdad akiwa na mkewe Melania.

Ziara hiyo ameifanya siku chache baada ya kutangaza kwamba anawaondosha wanajeshi wa Marekani kutoka Syria na kupunguza wanajeshi wa Marekani huko Afghanistan.

Akizungumza na wanajeshi alitetea msimamo wake huo unaopingwa na wakuu wa jeshi na kukosolewa na wanasiasa wa pande zote hapa Marekani.

Sisi hatufanyi kazi ya kujenga taifa. Kukarabati Syria kutahitaji suluhisho la kisiasa na ni suluhisho ambalo linabidi kugharimiwa na majirani zake tajiri, na sio Marekani. Wacha wagharimia na watalipa.

Alipokuwa anarudi nyumbani Trump alisimama kwa muda mfupi katika kambi ya kijeshi ya Marekani ya Ramstein nchini Ujerumani na kuzungumza na wanajeshi huko.

Ziara hii inafanyika pia baada ya kiongozi huyo kulaumiwa kiutowatembelea wanajeshi wa Marekani katika maeneo ya vita kama walivyofanya viongozi walomtangulia.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG