Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:29

Jim Mattis anajiuzulu kama waziri wa ulinzi Marekani


Jim Mattis, waziri wa ulinzi wa Marekani
Jim Mattis, waziri wa ulinzi wa Marekani

Taarifa zimekuja siku moja baada ya Rais Trump aliposema vikosi vya Marekani vitaondoka Syria hatua ambayo Pentagon iliipinga.Trump alisema Mattis anastaafu huku Mattis aliwasilisha barua Pentagon inayoeleza kwamba anajiuzulu.

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza Alhamis kwamba waziri wa ulinzi Marekani, James Mattis ataondoka kwenye nafasi hiyo Februari mwakani.

Rais Trump aliandika ujumbe kwenye Twitter unaosomeka “Jenerali Jim Mattis atastaafu mwishoni mwa Februari huku kukiwa na tofauti ya mitazamo baada ya kuhudumu kwenye utawala wangu kama waziri wa ulinzi kwa miaka miwili iliyopita. Katika kipindi cha uongozi wake kuna mafanikio mazuri yamefikiwa hususan heshima katika ununuaji wa vifaa vipya vya mapigano”. Rais Trump aliandika maneno mengi na kisha alimaliza kwa kuandika “namshukuru Jim kwa utoaji wake huduma kwenye wadhifa huo”.

Taarifa hizo zimekuja siku moja baada ya Rais Trump aliposema kwamba vikosi vya Marekani vitaondoka Syria hatua ambayo Pentagon iliipinga. Wakati Trump aliposema Mattis alikuwa anastaafu, Mattis aliwasilisha barua Pentagon inayoeleza kwamba alikuwa anajiuzulu.

Sarah Sanders, msemaji wa White House
Sarah Sanders, msemaji wa White House

Wakati huo huo msemaji wa White House, Sarah Sanders aliwaambia waandishi wa habari siku ya Alhamis kwamba Rais Trump na Mattis wanafanya kazi vizuri licha ya kutokukubaliana juu ya sera za mambo ya nje na masuala mengine.

XS
SM
MD
LG