Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alikuwa mwenyeji Jumamosi wa viongozi kutoka Ufaransa, Ujerumani na Russia kwenye mkutano unaowashirikisha viongozi wane mjini Instanbul unaozungumzia juu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
Mkutano huo unalengo la usitishaji mapigano kati ya waasi wa Syria na vikosi vya serikali mpango ulioandaliwa na Moscow na Ankara. Kabla ya kukutana kwao Rais Erdogan alifanya mazungumzo ya faragha na Rais wa Russia Vladimir Putin na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel. Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa juu ya mazungumzo yao.
Msemaji wa rais wa uturuki alisema Ijumaa kwamba lengo la mkutano huo ni kufafanua hatua zilizohitajika kuunda suluhisho la kisiasa kwa ajili ya mgogoro wa Syria. Washirika wakuu wawili wengine katika mgogoro wa Syria, Marekani na Iran hawahudhurii mkutano huu.