Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:51

Makombora ya Iran nchini Syria


Makombora ya Iran kutoka mji wa Kermanshah yakilenga wapiganaji wa Islamic State nchini Syria.
Makombora ya Iran kutoka mji wa Kermanshah yakilenga wapiganaji wa Islamic State nchini Syria.

Marekani imekosoa shambulizi la makombora lililotekelezwa na Iran dhidi ya wapiganaji mashariki mwa Syria, ikilitaja kuwa shambulizi la uchokozi, lisilozingatia kanuni zilizopo pamoja na lisilo salama.

Msemaji wa Pentagon kamanda Sean Robertson, ameambia sauti ya Amerika kwamba Iran haikuchukua hatua za kuarifu nchi nyingine zinazofanya shughuli za kijeshi nchini Syria, kabla ya shambulizi lake la Jumatatu.

Jeshi la ulinzi la Iran limesema kwamba makombora sita yalishambuliwa kutoka mkoa wa kaskazini magharibi mwa mkoa wa Kermanshah, kupita juu ya miji iliyo katikati mwa Iraq na kulenga sehemu zilizo mashariki mwa Syria katika mji wa Albu Kamal, karibu na mpaka wa Iraqi.

XS
SM
MD
LG