Iran yailaumu Israel kufuatia kukatika umeme kituo cha nyuklia

Rais wa Iran Hassan Rouhani (wapili kutoka kulia) anamsikiliza mkuu wa Taasisi ya Atomic ya Iran Ali Akbar Salehi alipokuwa akitembelea kuona maonyesho ya mafanikio ya nyuklia huko Tehran, Iran.

Iran inailaumu Israel kwa kukatika umeme katika kituo chake cha nyuklia cha Natanz.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Saeed Khatibzadeh, alisema machine za usindikaji wa Uranium ziliharibiwa, na kwamba Iran italipiza kisasi kisichojulikana dhidi ya Israel.

Mkuu wa nyuklia wa Iran, Ali Akbar Salehe, aliliita tukio la Jumapili, kitendo cha ugaidi wa nyuklia.

Idara ya kimataifa wa nishati ya Atomic, ya Umoja wa Mataifa ambayo inafuatilia program ya atomic ya Iran, ilisema Jumapili kwamba ilikuwa inafahamu hali hiyo na inafuatilia maendeleo yake.

Hata hivyo haikufafanua kwa kina juu ya suala hilo. Ikiwanukuu maafisa wawili wa ujasusi ambao walisema walikuwa wamejulishwa juu ya uharibifu.

Wakati huo huo gazeti la New York Times, liliripoti kuwa tukio hilo lilikuwa pigo kubwa kwa Iran kuweza kusindika Uranium, na inaweza kuchukua hadi miezi tisa kurejesha tena kiwanda cha Natanz.