Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:56

Wananchi wa Iraq waandamana kuwakumbuka Soleimani na al-Mohandes


Maelfu ya wananchi wa Iraq walikusanyika katika uwanja wa Tahrir Square ulioko katikati ya mji wa Baghdad JumapiliJan. 3, 2021.
Maelfu ya wananchi wa Iraq walikusanyika katika uwanja wa Tahrir Square ulioko katikati ya mji wa Baghdad JumapiliJan. 3, 2021.

Maelfu ya wananchi wa Iraq walikusanyika katika uwanja wa Tahrir Square ulioko katikati ya mji wa Baghdad Jumapili kuadhimisha mwaka mmoja tangu mauaji ya watu wawili yaliyofanywa na shambulizi la anga la Marekani, mmoja ni jenerali wa ngazi ya juu wa Iran na kiongozi wa kikundi cha wanamgambo wenye nguvu wa dhehebu la Shia.

Shambulizi la mwaka 2020 la Marekani lililofanywa kwa kutumia ndege zisizo kuwa na rubani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad lilimuua Meja Jenerali Qasem Soleimani, kamanda wa Kikosi Maalum cha Quds cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRGC) na Abu Mahdi al-Mohandes, naibu kiongozi wa wanamgambo wa kikundi cha Hashd al-Shaabi cha Iraq, pamoja na wanamgambo washirika wengine kadhaa wa Iran.

Wananchi wa Iran wakiandamana kulaani mauaji ya Qasem Soleimani, Tehran January 3, 2020.
Wananchi wa Iran wakiandamana kulaani mauaji ya Qasem Soleimani, Tehran January 3, 2020.

Wengi kati ya waandamanaji walikuwa wamebeba mabango ya picha za Soleimani na al-Mohandes huku wengine wakidai kufukuzwa kwa vikosi vya Marekani nchini Iraq.

Maelfu ya waombolezaji waliandamana katika barabara kuu inayoelekea uwanja wa ndege wa Baghdad jioni ya Januari 2 kuwaenzi Soleimani na al-Mohandes na wengine 10 waliouliwa katika shambulizi la Marekani.

Sehemu ya shambulizi hilo la Marekani kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani imegeuzwa kuwa uwanja mtakatifu uliotengwa kwa kuwekwa kamba nyekundu, kumewekwa picha ya Soleimani na al-Muhandis katikati, huku waombolezaji wakiwasha mishumaa.

Mauaji ya Soleimani yalizua hofu juu ya kutokea mgogoro wa kijeshi kati ya Marekani na Iran.

Mivutano kati ya Washington na Tehran imeongezeka tangu Rais wa Marekani Donald Trump alipojitoa katika mkataba wa nyuklia wa Iran mwaka 2018 na kurejesha vikwazo vikali vya uchumi kwa Iran.

Wakati Soleimani alipouliwa, Trump aliposti ujumbe wa Twitter kuwa Wairan walikuwa “wamewaua au kuwajeruhi vibaya sana maelfu ya Wamarekani kwa kipindi kirefu na walikuwa wanapanga kuuwa zaidi.”

Iran ilijibu mauaji hayo ya viongozi hao wawili kwa kurusha makombora katika kambi za kijeshi nchini Iraq yenye vikosi vya Marekani.

Hatua za usalama zimeimarishwa nchini Iraq na vikosi vya usalama vimepelekwa kwa idadi kubwa. Wizara ya Mambo ya Ndani imesema Januari 2 kuwa mpango maalum ulikuwa umeandaliwa kuwalinda waandamanaji.

Hatua za usalama pia ziliongezwa katika maeneo yaliyo karibu na eneo la Green Zone mjini Baghdad, ambalo lina ofisi za balozi za nje na ofisi za serikali.

Kwa wiki kadhaa, maafisa wa Marekani wanahisi kuwa Iran au washirika wanamgambo wangeweza kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuuwawa kwa Soleimani Januari 3.

Januari 2, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alimsihi Trump kutoingia katika “mtegoni” kwa kutumia kile kinachodaiwa kuwa ni mpango wa Israeli wa kuchochea vita kwa kushambulia vikosi vya Marekani nchini Iraq.

“Habari mpya za kijasusi kutoka Iraq zinaonyesha kuwa mamluki wa Israeli wanapanga njama za mashambulizi dhidi ya Marekani – na kumfanya Trump ambaye yuko njiani kumalizika muda wake wa uongozi kuamini uongo utakao halalisha kitendo cha kuanzisha vita,” amesema Zarif katika ujumbe wa Twitter.

Siku moja baadae, afisa wa Israeli aliluuza madai kuwa nchi yake ilikuwa inajaribu kuirubuni Marekani kuanzisha vita dhidi ya Iran na kusema ni “upuuzi.”

Ni Israeli ndiyo inatakiwa kuchukua tahadhari kwa uwezekano wa mashambulizi ya wairan katika maadhimisho yam waka mmoja tangu Soleimani kuuwawa, Waziri wa Nishati Yuval Steinitz amesema katika radio ya umma ya Kan Januari 3.

XS
SM
MD
LG