Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:55

Kiongozi wa Kishia wa juu Iraq alaani mashambulizi dhidi ya waandamanaji


Ayatollah Ali Sistani
Ayatollah Ali Sistani

Kiongozi wa kidini wa dhehebu la Kishia Ijumaa amelaani mashambulizi yaliyo sababisha mauaji dhidi ya waandamanaji wanaopinga serikali, akikemea vikosi vya usalama kwa kutokuchukua hatua zaidi kuzuia machafuko katika viwanja ambako maandamano yanafanyika nchini kote.

Waandamanaji wanane waliuawa wiki hii katika mashambulizi yaliowalenga makundi ya waandamanaji yaliofanywa na wafuasi wa kiongozi maarufu wa kidini Moqtada Sadr, waliokuwa pia katika mji mtukufu wa Najaf – nyumbani kwa kiongozi wa dhehebu la Kishia.

Katika hutba ya kila wiki ya Ijumaa iliyotolewa na mwakilishi, Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Sistani alilaani umwagaji wa damu kuwa kitu “kinachouma na balaa” na kusema vikosi vya usalama vya taifa ni “muhimu” kwao kuhakikisha nchi “haitumbukii katika shimo la vurugu”

“Hakuna uhalali wowote kwa vikosi hivyo kuacha kutekeleza majukumu yao katika suala hili, au kwa mtu yoyote kuwazuia kufanya hivyo,” amesema Sistani.

“Ni lazima watekeleze majukumu ya kuimarisha utulivu na usalama, kuwalinda wanaoandamana kwa amani na maeneo wanayokusanyika, wawatambulishe wale wakandamizaji na wanaojipenyeza kufanya vurugu, na kulinda maslahi ya raia wasifikiwe na wale wote wanaofanya mashambulizi ya hujuma.

Mapema wiki hii, Sadr amewataka wafuasi wake kuhakikisha shule barabara na ofisi za serikali zinafunguliwa ambazo zilifungwa kwa miezi kadhaa kutokana na maandamano.

Takriban watu 490 wameuawa katika vurugu zinahusiana na maandamano tangu mwezi Oktoba, wakati maandamano yalipozuka mjini Baghdad na eneo lote la kusini lenye wafuasi wa dhehebu la Kishia waliowengi akishinikiza kufanyika mabadiliko ya viongozi wa kisiasa.

XS
SM
MD
LG