Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:05

Vyombo vya habari vya serikali Iran vyapotosha taarifa za mashirika ya habari ya Magharibi juu ya hutba ya Khamenei


Waumini wakisikiliza hotuba ya kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alipokuwa akiongoza ibada ya sala ya Ijumaa katika msikiti mkuu wa Tehran.
Waumini wakisikiliza hotuba ya kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alipokuwa akiongoza ibada ya sala ya Ijumaa katika msikiti mkuu wa Tehran.

Vyombo vya habari vya serikali nchini Iran vimepotosha habari zilizo tangazwa na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi juu ya hotuba ya Ijumaa ambayo ni nadra kutolewa na kiongozi wa juu wa Iran.

Vyombo hivyo vimepuuzia jinsi vyombo vya habari vya Magharibi vilivyo gusia yale yanayofahamika kama mapungufu ya kiongozi huyo katika kukabiliana na matatizo ya ndani ya nchi hiyo.

Ayatollah Ali Khamenei aliongoza ibada ya sala ya Ijumaa mjini Tehran kwa mara ya kwanza tangu aliposita kufanya hivyo mwaka 2012, akitoa hutba katika Msikiti Mkuu wa mji mkuu Tehran. Kiongozi huyo wa juu kwa muda mrefu amekuwa anatoa hotuba hizo kwa umma pale tu kunapotokea misukosuko ya kitaifa siku za nyuma.

Katika hotuba yake aliikosoa Marekani na Washirika wake wa Ulaya ikiwemo Uingereza, Ufaransa na Ujerumani. Aliwadhihaki viongozi wa Marekani kama “vikaragosi” wakidai kuwa wanasimama na wananchi wa Iran lakini kiuhakika wanataka “kuwachoma” wananchi wa Iran “visu venye sumu.”

Hutba ya Khamenei’s imekuja wiki mbili baada ya Marekani kufanya shambulizi la kujihami lililomuua jenerali wa juu Qassem Soleimani, katika uwanja wa ndege wa Baghdad.

Katika maelezo yake, Khamenei aliituhumu Marekani kwa kujihusisha na "ugaidi" kwa kumuua Soleimani, ambaye alikuwa anaongoza kikosi maalum cha Quds.

Pia alikuwa ameorodheshwa kama kiongozi wa jumuiya ya kigaidi iliyouwa mamia ya vikosi vya Marekani nchini Iraq na kuendesha vikundi vya wanamgambo vilivyokuwa vinapigana na Marekani na washirika wake katika eneo hilo.

Khamenei alisisitiza kwamba umati mkubwa wa watu, ulijitokeza, ili kuhudhuria mazishi ya jenerali wa jeshi aliyeuawa katika shambulizi lililotekelezwa na Marekani mapema mwezi Januari 2020.

Amesema pamoja na changamoto ambazo zinaendelea kuikabili nchi hiyo, inaonyesha jinsi raia wa Iran wanavyounga mkono utawala wake.

Amesema kwamba kifo cha Jenerali Qassem Soleimani, ni pigo kubwa kwa vita dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State, kwa sababu, kama kamanda, alionyesha uongozi bora katika kupambana na wanamgambo hao.

Katika siku za karibuni, kumeshuhudiwa maandamano makubwa kwenye barabara za Tehran, kufuatia kutunguliwa kwa Ndege ya shirika la Ndege la Ukraine, ambayo, viongozi wa Iran, wamekiri kwamba ilitunguliwa kwa makosa.

Watu wote 176 waliokuwa wakisafiri ndani ya ndege hiyo waliuawa. Sala ya Ijumaa ilihudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Iran, mara kwa mara walikatiza hotuba yake wakisema, Mungu ni Mkubwa.

XS
SM
MD
LG