Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:06

Trump aionya Iran baada ya Ubalozi wa Marekani kushambuliwa Iraq


Ubalozi wa Marekani nchini Iraqi katika Ukanda wa kimataifa Green Zone wenye ulinzi mkali Dec. 20, 2020, ambapo inadaiwa kuwa wanamgambo wenye mafungamano na Iran walilishambulia kwa roketi.
Ubalozi wa Marekani nchini Iraqi katika Ukanda wa kimataifa Green Zone wenye ulinzi mkali Dec. 20, 2020, ambapo inadaiwa kuwa wanamgambo wenye mafungamano na Iran walilishambulia kwa roketi.

Rais wa Marekani Donald Trump ameionya Iran kutofanya shambulizi lolote dhidi ya jeshi la Marekani au wanadiplomasia nchini Iraq, siku kadhaa baada roketi zinazoshukiwa kupigwa na wanamgambo wa Iraqi wanaoungwa na Iran kushambulia ubalozi wa Marekani mjini Baghdad katika eneo la Green Zone lenye udhibiti mkali.

Onyo lililotolewa katika ujumbe wa Twitter Desemba 23, limekuja baada ya maafisa wa juu wa usalama wa taifa wa Marekani walipokutana kuandaa njia mbadala kadhaa watakazo pendekeza kwa rais ili kuzuia shambulizi lolote katika maeneo yenye maslahi ya Marekani nchini Iraq.

Kile kinachoitwa kikundi cha kamati muhimu, ambacho kinamjumuisha kaimu Waziri wa Ulinzi Chris Miller, Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo, na mshauri wa usalama wa taifa Robert O’Brien walikutana White House, shirika la habari la Reuters limeripoti, likimnukuu afisa ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Kwa wiki kadhaa, maafisa wa Marekani wamependekeza kuwa Iran au wanamgambo washirika wake nchini Iraqi wanaweza kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi ili kuadhimisha mwaka mmoja wa shambulizi la droni ya Marekani iliyomuua jenerali wa ngazi ya juu wa Iran, Qasem Soleimani, na viongozi wa wanamgambo wa Iraqi nje ya uwanja wa ndege wa Baghdad Januari 3.

Lengo la mkutano wa White House ilikuwa “kutayarisha mapendekezo kadhaa yaliyo sahihi ambayo tunaweza kuyawasilisha kwa rais ili kuhakikisha kuwa tunawazuia wairani na wanamgambo wa Kishia nchini Iraq kufanya mashambulizi kwa wafanyakazi wetu,” afisa mwandamizi ameiambia Reuters.

Kufuatia mkutano huo, Trump aliandika maoni katika mtandao wa Twitter kuzungumzia shambulizi la roketi lililokuwa limelenga eneo lenye ulinzi mkali la Green Zone mjini Baghdad Disemba 20, lililosababisha uharibifu mdogo katika eneo la ubalozi wa Marekani na eneo la makazi katika ukanda wa kimataifa.

“Ubalozi wetu mjini Baghdad ulipigwa na roketi kadhaa Jumapili. Roketi tatu zilifeli. Fikiria zilikuwa zinatoka wapi : IRAN,” Trump aliandika juu ya picha inayodai kuonyesha roketi hizo ni kutoka Iran.

XS
SM
MD
LG