Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:08

Marekani yaweka vikwazo zaidi kwa Iran


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo, akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari akitangaza vikwazo zaidi kwa Iran.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo, akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari akitangaza vikwazo zaidi kwa Iran.

Marekani, Jumatatu imeweka vikwazo vingine dhidi ya Iran, kukabiliana na mipango ya Tehran ya nyuklia, makombora na uzalishaji wa silaha wenye utata.

Vikwazo hivyo ni kukabilina na kitisho cha Tehran, na kuifanya Washington kutaka vikwazo zaidi vya Umoja wa Mataifa kwa Iran ambavyo havikukubaliwa Jumamosi iliyopita.

Mshauri wa usalama wa taifa wa White House, Robert O’Brien, amesema Jumatatu kwamba utawala wa rais wa Marekani, Donald Trump, unaweka vikwazo vipya kwa Iran.

Vikwazo hivyo vinajumuisha kudhibiti biashara 27, na watu wanaohusiana na programu za silaha za nyuklia wa Iran.

Amri ya kiutendaji ya White House inaelezea mipango ya kuzuia mali za watu wanao husika kusafirisha mali ghafi za silaha, na vifaa vya jeshi kwenda na kutoka Iran.

Wizara za mambo ya nje na biashara za Marekani, pia zimeelezea namna raia hao wa kigeni, na biashara zitakavyo kabiliwa na vikwazo.

XS
SM
MD
LG