Ethiopia : Jenerali Seare Monnen auawa katika jaribio la mapinduzi

Jenerali Seare Monnen

Kiongozi wa Jeshi la nchini Ethiopia,Jenerali Seare Monnen, ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake nchini Ethiopia.

Vyanzo vya habari vimesema yeye na afisa mwingine walipoteza maisha katika mji wa Amhara wakijaribu kudhibiti mapinduzi dhidi ya utawala, Waziri Mkuu Abiy Ahmed alisema mjini Addis Ababa nchini Ethiopia..

Mjini Ahmara, Gavana wa mji huo Ambachew Mekonnen aliuawa pamoja na mshauri wake.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yameikumba Amhara na miji mingine miaka ya hivi karibuni.

Waziri Mkuu alikwenda kwenye kituo cha Televisheni akiwa na mavazi ya kijeshi kukemea mashambulizi hayo.

Tangu uchaguzi wa mwaka 2018 Abiy amekuwa akifanya juhudi kumaliza mvutano wa kisiasa kwa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, kuondoa makatazo dhidi ya vyama vya kisiasa na kuwashtaki maafisa wanaoshutumiwa kukiuka haki za binadamu.

Wakati huohuo Marekani imewatahadharisha wafanyakazi wake mjini Addis Ababa kubakia majumbani mwao, ikisema ina taarifa za kiintelijensia kuhusu mashambulizi ya risasi siku ya Jumamosi.