Familia ya George Kabau aliyepoteza maisha katika ajali ya ndege ya Ethiopia akiwa na umri wa miaka 29 inataka kampuni ya Boeing kutoa taarifa na mawasiliano ya barua pepe ikitoa taarifa kamili juu ya uchunguzi wa ajali hiyo inayohusu ndege yake ya 737 Max 8.
Pia Aprili 4, 2019, familia ya Samya Stumo, kupitia mawakili wake walifungua kesi dhidi ya kampuni ya Boeing, Aprili 4, 2019reacts during a news conference in Chicago where attorneys for the family announced a lawsuit against Boeing, April, 4, 2019.
Mashirika ya ndege kote duniani, yamesitisha matumizi ya ndege aina ya 737 Max 8 baada ya ajali ya Ethiopia iliyouwa watu 157.
Wakati huohuo Wizara ya Mambo ya Nje nchini Kenya imezitaka familia za wahanga wa ajali hiyo ya Shirika la Ndege la Ethiopia kutafuta kibali cha uwakilishi kutoka mahakamani ili waweze kupata fidia.
Kibali cha uwakilishi ni waraka unaothibitisha haki ya kisheria na uwezo wa kushughulikia mali ya mtu ambaye amekufa. Kinamruhusu aliyepewa kibali hicho kusimamia malipo ya mtu aliyekufa.
"Wizara hiyo inapenda kuzishauri familia na ndugu wa wale waliokufa katika ajali ya ndege ET 302 Machi 10, wakati wako Kenya, kuchukua waraka huo kutoka mahakama za Kenya kama inavyotakiwa na sheria ya kurithi ya Kenya, ili waweze kupata fidia kutoka shirika la ndege la Ethiopia," Katibu Mkuu Michael Kamau amesema Jumatano.
Mchakato huu unakusudia kuhakikisha kuwa wale tu wanaostahiki malipo, ikiwa ni wenye waraka wa mirithi au barua ya usimamizi wa mali ya marehemu, waweze kupata fidia."