Ajali ya Ethiopian Airlines : Watu 157 wapoteza maisha

Familia za waliopoteza maisha katika ajali ya Ethiopian Airlines wakiwa katika huzuni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Addis Ababa, Jumapili, Machi 10, 2019.

Shirika la ndege la Ethiopian Airlines iliyokuwa ikiruka kutoka Addis Ababa imeanguka muda mfupi baada ya kuruka Jumapili, asubuhi, na kuua watu 157 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Shirika la habari la serikali ya Ethiopia limesema kuwa ndege hiyo iliyoanguka karibu na mji wa Bishoftu lilikuwa na abiria kutoka nchi 33.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737-Max 8 ilikuwa ni ndege mpya, iliyokabidhiwa kwa shirika la ndege la Ethiopia, kwa mujibu wa takwimu za kampuni ya Planespotters Civil aviation.

Boeing imetoa tamko la mstari mmoja Jumapilli, ikisema kuwa " Boeing inataarifa za ajali hiyo ya ndege na inafuatilia kwa ukaribu kabisa."

Kampuni ya Flightradar inayofuatilia urukaji wa ndege kupitia akaunti yake ya Twitter imesema kuwa "spidi ya kuruka" wakati ikiondoka uwanja wa ndege ya ndege hiyo ya Ethiopia "ilitetereka baada ya kuruka.

Boeing 737-MAX 8 inafanana na aina ya ndege iliyoruka Oktoba kutoka Jakarta na kuanguka katika Bahari ya Java baada ya dakika chache, na kuua watu wote 189 waliokuwa katika ndege hiyo ya Lion Air.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.