Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:11

WHO yatahadharisha janga kubwa zaidi Afrika kutokana na COVID-19


Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameonya kufungwa kwa mipaka ya nchi na kusitisha shughuli zote ili kupambana na janga la COVID 19 kunaweza kusababisha kuongezeka kwa vifo kutokana na ugonjwa wa Malaria katika nchi za Afrika.

Mkurugenzi huyo anasema uchambuzi mpya uliochapishwa wiki iliyopita unakadiria kwamba kusitishwa kwa huduma muhimu za afya hasa za Malaria kutaweza kusababisha madhara makubwa na pengine kushuhudiwa idadi kubwa ya vifo barani humo.

Mbali na ugonjwa wa Malaria, mkuu wa WHO anasema mataifa 21 kote duniani yanaripoti juu ya upungufu wa dawa za chanjo dhidi ya maradhi mbali mbali.

Ghebreyesus ameeleza kuwa karibu watu milioni 13 tayari wameathirika kutokana na kuchelewa kupata chanjo zao za kawaida.

Mkurugenzi huyo amesistiza tena wasiwasi wa WHO kutokana na kuongezeka kwa mambukizo ya magonjwa mbali mbali barani Afrika, Mashariki ya Ulaya, Amerika Kusini na baadhi ya nchi za Asia.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG