Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 04, 2025 Local time: 03:22

Wataalam : Marekani, washirika hawaelekei watakubali madai ya Russia


Rais wa Russia Vladimir Putin (Sputnik/Valeriy Sharifulin/Pool via Reuters)
Rais wa Russia Vladimir Putin (Sputnik/Valeriy Sharifulin/Pool via Reuters)

Russia isiitegemee Marekani na washirika wake kukubali madai yake ya karibuni yakutaka kuongezwa kwa seti ya “dhamana za kiusalama.” 

Madai hayo yanataka kupigwa marufuku upanuzi wa NATO na kusitisha kwa shughuli zote za kijeshi za muugano huo huko Ulaya Mashariki, eneo la Caucasus na Asia ya Kati, wataalamu na maafisa wa Marekani wamesema Ijumaa.

Marekani na washirika wake wa NATO, hata hivyo, wameashiria kwamba wanaweza kuwa tayari kuingia katika mazungumzo na Russia, hususan kama Kremlin itakubali kupunguza kiwango cha wanajeshi wake katika mpaka wake na Ukraine jambo ambalo limezusha wasiwasi kuhusu uwezekano wa kufanya uvamizi.

Marekani na NATO zilikuwa zinajibu rasimu za mikataba ambayo Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia iliwasilisha kwao mapema wiki hii na baadae kuitoa hadharani siku ya Ijumaa.

Rasimu hizo, ambazo ziliandaliwa bila ya mashauriano na Marekani na NATO, zitaulazimisha umoja huo kuacha kupelekea wanajeshi wa ziada katika nchi ambazo hazikuwa tayari na majeshi ya NATO mwaka 1997.

Nchi hizo ni pamoja na wanachama wa ushirika wa Ulaya Mashariki kama vile Poland, Hungary, Jamhuri ya Czech, nchi za Baltic na nyingine kadhaa za iliyokuwa jamhuri ya Soviet.

Pendekezo mkataba huo utazitaka pande mbili hizo kuweka viwango kwa upelekaji wa makombora ya masafa mafupi na ya kati na mazoezi ya kijeshi ya idadi kubwa ya kijeshi karibu na mpaka wa Russia.

XS
SM
MD
LG