Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 03:28

Uhusiano wa Russia na NATO waendelea kudorora, Stoltenberg


Katibu mkuu wa NATO,Jens Stoltenberg
Katibu mkuu wa NATO,Jens Stoltenberg

Katibu mkuu wa NATO Jenerali Jens Stoltenberg amesema Alhamisi kwamba uhusiano kati ya Russia na muungano huo umeshuka zaidi tangu kumalizika kwa vita baridi.

Stoltenberg ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa ulinzi wa NATO mjini Brussels. Hali ya taharuki imetanda kati ya Russia na NATO katika wiki za karibuni wakati taifa hilo likitangaza Jumatatu kwamba limesitisha uanachama wa kudumu kwenye muungano huo, yakionekana kuwa majibu ya kufukuzwa kwa maafisa wake wanane kutoka muungano huo mapema mwezi huu.

Wakati akihutubia wanahabari Alhamisi, Stoltenburg amesema kwamba amesikitishwa na hatua ya Russia ya kufunga ofisi ya NATO mjini Moscow. Ameongeza kusema kwamba bado kuna njia za kushauriana na Russia ingawa sio rahisi.

Kiongozi huyo pia amesema kwamba mataifa wanachama wanaendelea kutathmini upya kuhusu masuala ya ulinzi wa maeneo yao. Suala la Taliban la kuchukua udhibiti wa Afghanistan pia ni kipaumbele kwenye mkutano wa Brussels.

XS
SM
MD
LG