Hatua hii imechukuliwa kujibu madai ya harakati mbaya za kijasusi za Russia huko Ulaya, ambazo zimejumuisha mauaji, kujaribu kuua na milipuko, wamesema maafisa wa Ulaya.
Wanadiplomasia hao wameambiwa waondoke Brussels mwishoni mwa mwezi huu.
Nafasi nyingine mbili za kidiplomasia za Russia ambazo sasa ziko wazi katika makao makuu ya NATO hazitaruhusiwa kujazwa, maafisa wa NATO waliiambia VOA.
Kufukuzwa kwa wanadiplomasia wanane wa Russia, kuliripotiwa kwanza na Sky News ya Uingereza, kulishutumiwa haraka na wabunge wa nchi hiyo.
Wabunge hao walisema Kremlin italipiza kisasi, ingawa sio lazima iwe vile vile kwa kutaka kuwafukuza wanadiplomasia wa Magharibi walioko Moscow, lakini wakiweka mazingira ya kuzorota zaidi kwa uhusiano kati ya nchi za Magharibi na Russia na kukumbusha kipindi cha vita baridi.