Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:35

Warussia wapiga kura huku madai ya dosari za uchaguzi yakijitokeza


Mwanamke akipiga kura katika kituo cha kupiga kura siku ya mwisho ya uchaguzi uliodumu kwa siku tatu huko Moscow, Russia, Sept. 19, 2021.
Mwanamke akipiga kura katika kituo cha kupiga kura siku ya mwisho ya uchaguzi uliodumu kwa siku tatu huko Moscow, Russia, Sept. 19, 2021.

Wananchi wa Russia wanapiga kura Jumapili katika siku ya mwisho ya uchaguzi wa bunge wa siku tatu uliogubikwa na madai ya kusambaa kwa dosari mbalimbali na msako mpya kwa harakati za mwanasiasa mpinzani Alexey Navalny aliyefungwa jela.

Utawala wa chama cha United Russia kinachoungwa mkono na Kremlin kinatarajiwa kushinda kura katika bunge, kufuatia kukamatwa kwa wapinzani na hivyo kuwaondoa wakosoaji katika ucahguzi na kuvizima vyombo vya habari huru.

Lakini chama kinachomuunga mkono Rais Vladimir Putin kiko hatarini kupoteza wingi wa viti katika bunge, wakati ukusanyaji maoni kabla ya uchaguzi ulionyesha umaarufu wake ukishuka kufikia kiasi cha asilimia 30.

Wingi sasa wa United Russia katika bunge wa robo tatu katika Bunge lenye viti 450 unakipa chama hicho nguvu za kupindukia, ikiwemo uwezo wa kubadili katiba kama ilivyofanya mwaka 2020 ili kumruhusu Putin kugombea mihula miwili zaidi ya urais baada ya 2024.

The Communists, chama cha pili chenye nguvu zaidi, kiko katika nafasi ya kupata viti vingi zaidi kwa gharama ya chama cha United Russia.

Chama cha The Communists kinaendelea kuwa na nguvu kikiungwa mkono miongoni mwa warussia wazee lakini kinaweza kupata nguvu kipindi hiki kwa kuungwa mkono na wafuasi wa Navalny.

Mkakati wa Navalny umejikita katika juhudi ya upigaji kura wa Smart Voting – nyenzo iliyotangazwa kama njia kwa wapiga kura wanaompinga Putin kuwatambua wagombea ambao wana nafasi nzuri kumshinda mgombea wa United Russia ili upinzani usiweze kugawanyika.

Wagombea wengi waliotambuliwa na juhudi hizo za Smart Voting wanatokea chama cha Communist, japokuwa chama hiki na vingine viwili ndani ya bunge mara chache hupiga kura dhidi ya juhudi za waliowengi au zile zinazosukumwa wazi na Kremlin.

“Iwapo chama cha United Russia kitashinda, nchi yetu itakabiliwa na miaka mitano mingine ya umaskini, miaka mitano ya ukandamizaji wa kila siku, na miaka mitano iliyopotea bure,” ujumbe wa Instagram wa akaunti ya Navalny ulisomeka hivyo katika mkesha wa uchaguzi.

Katika miezi ya hivi karibuni, mamlaka zimeanzisha kamatakamata ya jumla dhidi ya mtandao wa siasa wa Navalny, ukiitaja “taasisi ni taasisi yenye mkali” na kuwazuia wafuasi wa wanasiasa kushiriki katika uchaguzi,

Wakati upigaji kura ukianza Septemba 17, app ya muongozo wa uchaguzi iliondolewa kutoka mtandao wa Apple na Google katika kile wafuasi wa Navalny wamekemea kuwa ni udhibiti na kukubali shinikizo la Kremlin.

Vyanzo vya habari hii ni RFE/RL's Russian Service, Current Time, AP, na Reuters

XS
SM
MD
LG