Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:29

Chama tawala United Russia chadai kushinda viti theluthi mbili


Watu wakisubiri kupiga polling station during parliamentary elections, in Moscow, Russia, Sept. 17, 2021.
Watu wakisubiri kupiga polling station during parliamentary elections, in Moscow, Russia, Sept. 17, 2021.

Chama tawala kinachoungwa mkono na Kremlin cha United Russia kimedai kimeshinda theluthi mbili katika bunge kuu la Russia.

Kauli hiyo ya ushindi imekuja baada ya siku tatu za upigaji kura zilizogubikwa na madai ya wapinzani juu ya kuongezeka kwa ukiukwaji na wizi katika karatasi za kupigia kura.

Uchaguzi huo unaonekana kwa kiasi kikubwa kama sehemu muhimu ya juhudi za Rais wa Russia Vladimir Putin za kuimarisha nguvu zake kabla ya uwezekano wa uchaguzi katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2024, na kufanya udhibiti wa bunge la Russia au Duma kuwa muhimu.

Kura hiyo pia imegubikwa na ukosefu wa upinzani mkubwa baada ya mamlaka kutangaza kuwa taasisi zenye uhusiano na mfungwa Aleksei Navalny kuwa ni zenye msimamo mkali, na kumzuia mtu yeyote kutoka kwenye mtandao wake kugombea.

Kwa mara ya kwanza tangu 1993, waangalizi wa uchaguzi kutoka Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) hawakuwepo kwa sababu ya udhibiti uliowekwa na maafisa wa Russia.

XS
SM
MD
LG