Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:00

Kiongozi wa al-Qaida aliyevuma amefariki atokea katika video ya Septemba 11


 Ayman al-Zawahri
Ayman al-Zawahri

Kiongozi wa al-Qaida Ayman al-Zawahri ameonekana katika kanda mpya ya video kuadhimisha miaka 20 ya mashambulizi ya Septemba 11, miezi kadhaa baada ya uvumi kuenea kuwa alikuwa amefariki.

Kikundi cha SITE Intelligence Group ambacho kinafuatilia tovuti za wanajihadi kimesema video hiyo ilitolewa Jumamosi. Katika video hiyo, al-Zawahri amesema kuwa “Jerusalem kamwe haitageuzwa ya Wayahudi,” na kupongeza mashambulizi ya al-Qaida ikiwemo lile ambalo liliwalenga wanajeshi wa Russia nchini Syria mwezi Januari.

SITE imesema al-Zawahri pia alielezea kuondoka kwa majeshi ya Marekani kutoka Afghanistan baada ya miaka 20 ya vita. Imeongeza kusema kuwa katika maoni yake haionyeshi dalili muhimu ya kuwa yamerikodiwa hivi karibuni, kwani mkataba wa kuondoka majeshi ya Marekani uliosainiwa na Taliban mwezi Februari 2020.

Al-Zawahri hakutaja hatua ya Taliban kuikamata Afghanistan na mji mkuu Kabul mwezi uliopita, SITE imeongeza. Lakini alitaja shambulizi la Januari 1, lililowalenga wanajeshi wa Russia katika ukingo wa mji wa kaskazini mwa Syria wa Raqqa.

Uvumi umeenea tangu mwishoni mwa mwaka 2020 kuwa al-Zawahri alifariki kutokana na maradhi. Tangu wakati huo, hakuna video au ushahidi wa kuwa uliotolewa kuonyesha yuko hai, hadi jana Jumamosi.

“Kuna uwezekano alishafariki, itakuwa wakati fulani mwezi Januari 2021 au baada ya hapo,” mkurugenzi wa SITE, Rita Katz ameandika katika mtandao wa Twitter.

Video ya hotuba ya Al-Zawahri ilirekodiwa kwa dakika 61, sekunde 37 ilitolewa na taasisi ya al-Qaida ya Sahab Media Foundation.

Katika miaka ya karibuni, al-Qaida imekabiliwa na ushindani katika duru za mahasimu wake ikiwa ni pamoja na kikundi cha Islamic State.

IS imepata umashuhuri kwa kukamata maeneo makubwa ya Iraq na Syria mwaka 2014, na kutangaza “ukhalifa” na kuongeza washirika wake katika nchi mbalimbali katika ukanda huo.

“Ukhalifa” wa IS ulizimwa nchini Iraq na Syria, japokuwa wanamgambo wake wanaendelea naharakati zao na kufanya mashambulizi.

Abu Bakr al-Baghdadi, kiongozi kivuli wa IS aliuawa na vikosi maalum vya Marekani katika shambulizi huko kaskazini magharibi mwa Syria Oktoba 2019.

Al-Zawahri, Mmisri, alifanywa kiongozi wa al-Qaida kufuatia kuuawa kwa Osama Bin Laden mwaka 2011 huko Abbottabad, Pakistan na wanajeshi makomando wa Majini wa Marekani.

XS
SM
MD
LG