Kilichofuata ni miaka 19, miezi 10 wiki tatu na siku mbili za vita vya Afghanistan na Wizara ya Ulinzi kuhesabu vifo vya wanajeshi wasiopungua 2,325 wa Marekani.
Hakuna anayejua ni raia wangapi waliuwawa. Septemba 11 mwaka 2021 Rais Joe Biden atajaribu kuweka mstari chini ya majengo hayo mawili, akitoa heshima zake katika maeneo matatu ambayo mateso yake yalisababisha vita virefu vya Marekani.
Vita ya dunia dhidi ya ugaidi, kama ilivyoitwa, vilienea zaidi katika taifa la Asia ya kati la Afghanistan na kufika hadi Iraq na pembe nyingine za ulimwengu mpaka barani Afrika.
Nchini Iraq mzozo huo uliwauwa karibu wanajeshi 4500 wa Marekani na maelfu ya raia.
Tangu uamuzi uliokuwa na utata wa kuondoa wanajeshi Afghanistan mwishoni mwa mwezi August, utawala wa Biden umechukua hatua ngumu ya kusitisha vita vilivyodumu kwa miaka 20 kwa kutoa vilelezo vingi ambavyo vinaweza kutoa mwangaza juu ya maadhimisho ya Septemba 11.
Lakini pia kudumisha umbali na serikali ya Taliban iliyochukua madaraka Afghanistan wakati Wamarekani walipoondoka.