Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 08:29

China kushirikiana na Afrika Kusini kujenga kiwanda cha chanjo


Chanjo ya COVID-19 inayotengenezwa na kampuni ya Sinovac Biotech Ltd China.
Chanjo ya COVID-19 inayotengenezwa na kampuni ya Sinovac Biotech Ltd China.

Kampuni ya kutengeneza dawa ya China, Sinovac Biotech, imeanza mazungumzo juu ya kujenga kiwanda cha kutengeneza dawa za chanjo nchini Afrika Kusini ikishirikiana na kampuni moja ya nchi hiyo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Numolux ya Afrika Kusini, Hilton Kleion alitangaza habari hizo lIjumaa walipokuwa wanazindua kampeni ya majaribio ya chanjo ya kupambana na ugonjwa wa COVID 19.

Majaribio ya chanjo hiyo yamefanywa na kampuni ya Sinovac kwa ajili ya watoto wadogo na wachanga huko Afrika ya kusini.

Akizungumza na waandishi habari hii leo Klein amesema Majaribio hayo ni kichocheo cha kujenga kiwanda cha kuzalisha dawa za chanjo Afrika Kusini kwa ushirikiano kati ya Sinovac na Numolux.

Kiwanda hicho kitatengeneza aina mbali mbali za chanjo mbali na ile ya COVID-19. Sinovac haijatoa tarifa bado kuhusiana na tangazo hilo.

XS
SM
MD
LG