Rais alisema hayo wakati akiwakumbuka watu waliokufa miaka 20 iliyopita.
Biden alikuwa seneta wakati huo watekaji nyara walipotumia ndege nne, kufanya mashambulizi mabaya sana ya kigaidi kwa taifa mwaka 2001.
Hivi sasa Biden anaadhimisha Septemba 11 kwa mara ya kwanza kama kamanda mkuu.
Rais anatoa heshima zake katika maeneo matatu, ambako ndege zilianguka, lakini atawaachia wengine kutoa hotuba.
Badala yake White House, ilitoa hotuba iliyorekodiwa jana Ijumaa, ambapo Biden alizungumzia "dhana halisi ya umoja wa kitaifa,” iliyoibuka baada ya mashambulizi, ambapo ilionekana ni “ushujaa kila mahali katika maeneo yaliyotarajiwa na yasiyotarajiwa.”
“Kwangu hilo ndio somo kuu la Septemba 11,” alisema. “Umoja ni nguvu yetu kubwa.” Biden aliwasili New York Ijumaa usiku, wakati anga ilipokua ikiangazwa na “Nuru ya heshima”, inayopiga mahala ambako minara hiyo ilipokuwa imesimama.
Kituo chake cha kwanza leo, kilikuwa kwenye kumbukumbu ya kitaifa ya Septemba 11, mahala ambapo minara miwili ya kituo cha biashara duniani iliangushwa, wakati dunia ikiangalia tukio hilo baya, kupitia kwenye televisheni.