Ziara ya kiongozi huyo ambayo imekuwa ikifanyiwa kazi kwa miezi miwili na ilicheleweshwa kwa sababu ya mashauriano kuhusu matukio huko Afghanistan.
Maafisa waandamizi katika utawala wa Marekani walisema ujumbe wa ziara hiyo ni nia ya dhati ya Marekani kwa uhuru wa Ukraine, uadilifu wa kieneo na matarajio ya Euro-Atlantiki.
Maafisa hao waliwaambia waandishi wa habari, ajenda zitajumuisha masuala ya usalama, sera ya nishati na hali ya hewa, pamoja na juhudi za kupambana na ufisadi nchini Ukraine.
Maafisa hao pia walisema pande hizo mbili, zitatangaza makubaliano kadhaa pamoja na msaada wa usalama kwa Ukraine, misaada ya kibinadamu kwa wale walioathiriwa na mgogoro wa Russia huko mashariki, na misaada inayohusiana na virusi vya Corona.