Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:08

WHO yahofia kutokea vifo 236,000 zaidi kutokana na Covid-19 Ulaya


Hans Kluge
Hans Kluge

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema linahofia kutokea vifo vingine vya watu 236,000 ifikapo Disemba 1 kufuatia ugonjwa wa COVID-19 , ikieleza wasiwasi kuhusu kuwepo kiwango kidogo cha kupokea chanjo na upelekeaji wa chanjo kwa kiasi kidogo katika nchi masikini.

Wiki iliyopita kulikuwa na ongezeko la asilimia 11 la vifo katika eneo, ubashiri wa kuamininika unatarajia vifo 236,000 huko Ulaya, ifikapo Disemba 1.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO upande wa Ulaya Hans Kluge amewaambia waandishi wa Habari.

Ulaya imeandikisha karibu vifo milioni 1.3 kutokana na COVID-19 hadi sasa.

Kati ya nchi wanachama 53 wa WHO Ulaya , 33 wamesajili kiwango cha matukio zaidi ya asilimia 10 katika wiki mbili zilizopita, amesema Kluge.

Kuenea kwa kiasi kikubwa cha maambukizi katika eneo, kunaleta wasiwasi mkubwa, hasa katika maeneo ambayo kuna kiwango kidogo cha upokeaji wa chanjo kwenye idadi ya watu wanaopewa kipaumbele katika nchi kadhaa.

Wakati huohuo karibu nusu ya watu katika bara la Ulaya wamepewa chanjo kamili, zoezi la kupokea chanjo katika eneo limeshuka, amesema Kluge.

XS
SM
MD
LG